Sikukuu hiyo
ni kumbukumbu ya tukio la kuzaliwa kwa yesu kristu ambalo lilitokea zaidi ya
miaka 2000 iliyopita katika bethlehemu ya Uyahudi.
Mkuu wa
jeshi la polisi wilayani Ngara mkoani Kagera Bw Mohamed Milanzi amewataka viongozi na wananchi kutoa
ushirikiano kwa jeshi hilo ili kuimarisha usalama katika kipindi cha sikukuu za
krismas na mwaka mpya.
OCD Milanzi ameagiza
wakuu wa vituo, na askari wa usalama barabarani kuhakikisha usalama unaimarika
katika wilaya hiyo pamoja na kuwataka viongozi na wananchi kutoa taarifa za watu ambao
wataonekana kusababisha uvunjifu wa amani ili hatua zichukuliwe.
OCD Milanzi amewatahadharisha madereva wa
vyombo vya moto kuacha kuendesha wakiwa
wamelewa ili kuepuka ajali.
Blog ya
Mwana wa Makonda nawatakia wasomaji wetu wote sikukuu njema ya X-mass na Mwaka
mpya wa 2013.
No comments:
Post a Comment