Hivi ndivyo Benki ya CRDB ilivyofungua Tawi lake la Benki ya CRDB Mjini Bujumbura nchini Burundi. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, December 12, 2012

Hivi ndivyo Benki ya CRDB ilivyofungua Tawi lake la Benki ya CRDB Mjini Bujumbura nchini Burundi.


Tawi la Benki ya CRDB  Mjini Bujumbura nchini Burundi.


Rais  wa Burundi Piere Nkurunziza akiwasili katika sherehe za ufunguzi rasmi wa Benki ya CRDB jijini Bujumbura, Burundi. Benki ya CRDB imekuwa Benki ya kwanza ya kizalendo kufungua tawi lake nchini Burundi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei akizungumza na Balozi wa Tanzania Nchini Burundi Dkt. James Nzagi (Kushoto) na  Katibu wa Benki hiyo Bwana John Rugambo(wa pili kushoto) na Meneja Mkuu wa Benki ya CRDB Nchini Burundi Bw. Bruce Mwile.

Rais wa Burundi Mheshimiwa Piere Nkurunziza akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Benki ya CRDB  nchini Burundi. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt.Charles Kimei.

Rais wa Burundi Mheshimiwa  Piere Nkurunziza akisalimiana na Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa Benki ya CRDB Tully Esther Mwambapa alipokuwa akiwasili katika sherehe hizo.

Mwamuziki maarufu  wa Burundi Nimbona Jean Pierre”KIDUMU” akitumbuiza kwenye hafla hiyo.

Wafanyakazi wa Benki ya CRDB nchini Burundi wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wenzao kutoka Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad