Taarifa kutoka
eneo la tukio zinasema kuwa mauaji hayo yalifanyika baada ya wananchi hao
kuvamia na kukichoma moto kituo cha polisi cha Mugoma wilayani humo baada ya
askari hao kudaiwa kumpiga risasi fundi wa pikipiki.
Kwa mujibu
wa mashuhuda, tukio hilo lilitokea mchana wakati askari kadhaa wa kitengo cha
usalama barabarani walipofika kwa fundi pikipiki huyo na kutaka kuichukua
pikipiki aliyokuwa akiitengeneza kwa madai kuwa ilikuwa na makosa.
Fundi huyo
aligoma na kueleza kuwa asubiriwe mwenye pikipiki ili kuepuka kudaiwa chombo
hicho cha usafiri.
Mashuhuda hao, walidai kuwa baada ya
mvutano wa muda mfupi, askari hao walifyatua risasi na kumpiga fundi huyo
mguuni na kifuani, hivyo kusababisha kifo chake.
Aliongeza
kuwa, tukio hilo liliwapandisha hasira wananchi na kuwafukuza askari hao
waliokimbilia katika kituo hicho cha polisi.
Wananchi hao waliamua kukichoma moto kituo hicho hatua
iliyosababisha askari waliokuwemo kutoka na kukimbia kila mmoja na muelekeo
wake.
Alisema kuwa
askari aliyetajwa kwa jina la Koplo Paschal alianguka wakati akijinusuru, hivyo
kuvamiwa na wananchi waliokuwa na zana mbalimbali za jadi ambazo walitumia
kumshambulia na kumuua papo hapo.
Wananchi hao
pia wanadaiwa kumfuata askari mwingine anayetajwa kwa jina la Pc Alex aliyekuwa
amekimbilia kwenye nyumba ya mwananchi mmoja na kumtoa kwa nguvu na kisha
kuanza kumshambulia hadi kumuua.
Tukio hilo
limetokea ikiwa ni siku ya soko katika eneo hilo la Mugoma linalopakana na nchi
jirani ya Burundi ambapo raia wa Tanzania na Burundi hukutana na kufanya
biashara jirani na kituo hicho cha polisi.
IGP Said
Mwema.
|
Aidha wamiliki
wa maduka katika eneo hilo la Mugoma
wilayani Ngara mkoani Kagera wamesita kufungua biashara zao kwa kile
kinachodaiwa kuwa ni kuogopa msako unaoendeshwa na askari wa Jeshi la Polisi kufuatia
tukio hilo la hapo .
Diwani wa
kata ya Mugoma Bw George Rubagora ameiambia radio kwizera kuwa wakazi wa eneo hilo wamekumbwa na hofu kutokana
na kukamatwa kwa watu wengi wakidaiwa
kuhusika kwenye tukio hlo na kwamba imewapelekea baadhi ya wakazi wa kata ya Mugoma Kukimbilia nchi jirani
wakihofia kukamatwa.
Kutokana na
kuchomwa moto kwa kituo hicho, nyaraka mbalimbali zinadaiwa kuteketea, huku
pikipiki na baiskeli kadhaa zilizokuwa kituoni hapo nazo zikiteketea.
Mkuu wa
Wilaya ya Ngara, Costa Kanyasu naye alithibitisha vifo vya askari hao na
kueleza kuwa wanaendelea kufanya uchunguzi kujua ukweli wa tukio hilo, ikiwa ni
pamoja na kujua kama askari hao ndiyo walimpiga risasi mwananchi huyo.
Katika hatua
nyingine mkuu wa wilaya ya Ngara Bw Costantine Kanyasu amelitaka jeshi la
Polisi kutumia weledi katika kuendesha msako huo kwa kuepuka kuwakamata
wasiohusika kwenye matukio hayo pamoja na kuwataka wanasiasa kuepuka kutoa
maneno ya uchochezi wakati huu msoko ukiwa unaendelea.
Aidha mpaka
sasa Watu 18 wanashikiliwa na jeshi la Polisi wakituhumiwa kuhusika na tukio hilo
la mauaji ya askari polisi wawili pamoja na kuchoma moto kituo cha polisi cha
Mugoma wilayani Ngara mkoani kagera .
Kamanda wa
Polisi wa mkoa wa Kagera Bw Philipo Karangi amesema watu hao 18 wamekatwa
katika msako unaoendelea kufanyika ili kuwabaini waliohusika katika matukio
hayo .
Duh, Ngara kama Syria.
ReplyDelete