Mwandishi wa
BBC John Solombi ameripoti kwamba utafiti mpya unaonyesha asilimia 27 ya
wanawake Tanzania wanafanya ngono kinyume na maumbile.
Mtafiti
Mwanasayansi Irene Mremi kutoka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya
Binaadamu nchini Tanzania (NIMR) ambaye aliwasilisha ripoti hiyo kwa niaba ya
watafiti wenzake wa NIMR amesema katika utafiti walioufanya umebaini asilimia
26.5 ya wanawake hukubali kuingiliwa kinyume.
Baadhi ya
wanawake kutoka Kinondoni Dar es salaam, Tanga, Makete na Siha wamekiri kufanya
ngono kinyume na maumbile ambapo Mremi amesema wanawake hao wamesema chanzo
kikubwa kinacho wapelekea kufanya ngono kinyume na maumbile ni kujipatia kipato
zaidi, Kuogopa kupata Mimba, kulinda usichana wao na baadhi ya mila na tamaduni
za baadhi ya makabila.
Amekaririwa
akisema “ Utafiti wetu uliwahusisha wasichana na wanawake wa rika kuanzia miaka
15 na kuendelea na kada tofauti katika jamii kama wanafunzi, wafanyakazi,
wahudumu bar, wauguzi, makahaba na akina mama wa nyumbani, katika maeneo hayo
watu 903 walijitokeza wakiwepo pia wanaume ambao walihusishwa katika utafiti
huo”
Wakati wa
utafiti huo wanawake 44 kati ya 166 waliohojiwa walisema wanafanya tendo la
kujamiiana kinyume na maumbile ambapo Tanga ndio kumeonesha kukithiri kwa
vitendo vya wanawake kufanya mapenzi kinyume na maumbile ukilinganisha na
Makete ambako bado kuna idadi ndogo.
Wanaume
waliohojiwa wamesema wanafanya kwa ajili ya kupata raha tu na imani ya kuwa
huko hakuna maambukizi ya VVU/UKIMWI na wamekua wakitumia mafuta ya aina
mbalimbali ilhali matumizi ya mipira ni hafifu kwani wakitumia mipira (Condom)
inapunguza raha.
Wanawake pia
wamedai baadhi ya tamaduni zao hasa maeneo ya Mwambao huko Tanga msichana
akiolewa na kukutwa usichana wake haupo (Bikira) ni aibu kwake na wazazi hivyo
hulazimika kufanya mapenzi kinyume na maumbile, huku suala la Mimba nalo
likichukua nafasi.
Watafiti hao
wamesema ufanyaji huo wa ngono kinyume na maumbile umekuwa ukisababisha
michubuko kirahisi na kuchangia maambukizi ya Ukimwi kwa kasi tofauti na
kutumia njia ya kawaida ya kujamiiana, wanawake wengi wanaofanya ngono kinyume
na maumbile wamekuwa wakipata shida wakati wa kujifungua kwa misuli yao ya
kushindwa kuhimili kusukuma mtoto.
Source:
Millardayo Blog
No comments:
Post a Comment