Mabingwa wa
Ulaya Chelsea imejiimarisha kileleni mwa Ligi Kuu ya Uingereza baada ya kuichapa mabao 4-1 timu ya Norwich wakiwa nyumabani darajani Stamford Bridge.
Grant Holt
aliifungia Norwich bao la kuongoza dakika ya 11, lakini Chelsea ilisawazisha
kupitia kwa Fernando Torres kabla ya Frank Lapard na Eden Hazard kufunga mabao
ya ushindi kipindi hicho hicho cha kwanza na Branislav Ivanovic kuhitimisha
karamu ya mabao ya ushindi wa 4-1 zikiwa zimebaki dakika 15.
Chelsea
imefikisha pointi 19, baada ya kucheza mechi saba na kuendelea kuongoza Ligi
Kuu ikiwazidi pointi nne mabingwa
watetezi, Man City ambao nao wameshinda bao
3 - 0 dhidi ya Sunderland kwa magoli
ya Kolarov (4), Aguero (59) na Milner (88).
Aidha
matokeo mengine ya Ligi hiyo soka Uingereza ni
West
Brom 3 - 2 QPR
Swansea 2 - 2
Reading
Wigan 2 - 2
Everton
Jumapili
Oktoba 7
[Saa
9 na Nusu Mchana]
Southampton
v Fulham
[Saa
11 Jioni]
Tottenham
Hotspur v Aston Villa
Liverpool
v Stoke City
No comments:
Post a Comment