Mabingwa wa Ulaya na Dunia, timu ya taifa ya
Hispania wameendelea kushika nafasi ya kwanza kwenye Listi ya viwango bora vya
soka Duniani vya FIFA/Coca Cola viliyotolewa
leo huku timu ya taifa ya Tanzania ikibakia nafasi ya 132 kwenye ubora huo huku
kwenye Kumi Bora ,Timu ya taifa ya Ureno
ikipanda na kushika namba 3, Uingereza ikiporomoka na sasa ipo nafasi ya 5
kutoka nafasi ya 3 mwezi uliopita.Barani Afrika Tembo wa Africa ,Ivory Coast ndiyo wapo juu na wapo nafasi ya 16 ambayo ni ile ile kama ilivyokuwa Mwezi uliopita.
Timu ya taifa ya Colombia wameingia Kumi Bora baada ya kupanda nafasi 13 huku Denmark na Croatia zikiporomoka kutoka Kumi Bora.
Aidha Brazil ambao ni mabingwa wa Dunia mara 5, wameporomoka nafasi mbili na sasa wapo nafasi ya 14.
KUMI NA TANO BORA FIFA/COCA COLA:
1 Spain
2 Germany
3 Portugal
4 Argentina
5 England
6 Netherlands
7 Uruguay
8 Italy
9 Colombia
10 Greece
11 Croatia
12 Russia
13 France
14 Brazil
15 Switzerland
![]() |
| Listi nyingine mpya itatolewa Novemba 7. |






No comments:
Post a Comment