Premier League: Liverpool 0 Arsenal 2 - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, September 02, 2012

Premier League: Liverpool 0 Arsenal 2



Leo Arsenal wakiwa ugenini huko Anfield wameipiga Liverpool Bao 2-0 kwa bao za wachezaji wao Lukas Podolski na Santi Cazorla ambazo zimewaacha Liverpool wakiwa hawajashinda hata Mechi moja ya Ligi Msimu huu baada ya Mechi 3.


Arsenal walipata bao la kwanza katika Dakika ya 31 pale Nahodha wa Liverpool Steven Gerrard alipotaka kupenyeza pasi kwa Luis Suarez akiwa karibu na boksi la Arsenal lakini pasi hiyo ilinaswa na Arsenal na  Arsenal wakawa wako mbele kwa bao moja baada ya mpira huo kupewa Santi Cazorla aliechomoka nao na kumpa pande Lukas Podolski ambae shuti lake la chini lilimshinda Kipa Pepe Reina.

Bao la pili la Arsenal lilifungwa katika ya Dakika ya 68 kwa shuti kali la Santi Cazorla na safari hii alikuwa Lukas Podolski aliempa pasi Santi Cazorla.


Mabingwa Manchester City wameshinda Mechi yao ya pili ya Ligi Kuu Uingereza Msimu huu kwa kuifunga Queens Park Rangers bao 3-1.

Huu ni ushindi wa pili kwa Manchester City  katika Mechi 3 za Ligi kwa Msimu huu ambazo waliifunga Southampton 3-2 na kutoka sare 2-2 na Liverpool.


Tottenham wakicheza kwao White Hart Lane wameendelea kupata matokeo ambayo si mazuri kwao kufuatia sare ya bao 1-1 na Norwich City hii ikiwa ni sare ya pili baada ya kufungwa Mechi ya kwanza ya Ligi Kuu Uingereza.



Spurs walipata bao lao mfungaji akiwa Mchezaji wao mpya Moussa Dembele akicheza Mechi yake ya kwanza kabisa na alifunga bao hilo zuri katika Dakika ya 69.

Norwich walisawazisha katika Dakika ya 85 kwa bao la Robert Snodgrass.

Tottenham walijikuta wakiwa Mtu 10 katika Dakika ya 90 baada ya Kiungo wao Tom Huddlestone kupewa Kadi Nyekundu kwa kile kilichoonekana ni rafu mbaya na Refa Mark Halsey lakini huenda hii ikafutwa akikata Rufaa.


Mchezaji Andy Carroll, akiichezea Timu yake mpya West Ham kwa mara ya kwanza, alitengeneza bao mbili wakati  timu ya West Ham walipoichapa  Fulham bao 3-0 kwenye Mechi ya Ligi Kuu iliyochezwa leo Uwanja wa Upton Park.


Bao zote 3 zilifungwa Kipindi cha Kwanza na wachezaji wake Kevin Nolan, Dakika ya 1,Winston Reid dk  ya 29 na Matt Taylor dk ya  41.


Michezo ya muda huu ni:

Southampton  2 v 1 Manchester United

Newcastle United  0 v 1 Aston Villa


Na matokeo unaweza kutazama kwa juu katika blogge hii.




No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad