Mchezaji Samatta aipeleka Mazembe Nusu Fainali. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, September 02, 2012

Mchezaji Samatta aipeleka Mazembe Nusu Fainali.

Huko Lubumbashi nchini DRC Straika mahiri wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta, alipiga bao la kwanza na kuisaidia Timu yake  ya TP Mazembe kuwachapa Vigogo wa Misri Al Ahly bao 2-0 na kutinga Nusu Fainali ya CAF CHAMPIONZ LIGI pamoja na Al Ahly.


Bao la Mbwana Samatta lilifungwa Dakika ya 48 na bao la pili lilipatikana Dakika ya 61 mfungaji akiwa Deo Kanda.


TP Mazembe  wamebakiza Mechi moja ya kukamilisha Ratiba na sasa wanaingia Nusu Fainali pamoja na Al Ahly kutoka Kundi B na kutoka Kundi A timu zilizofuzu kuingia Nusu Fainali ni Esperance ya Tunisia, ambao ni Mabingwa watetezi pamoja na Sunshine Stars ya Nigeria.




MSIMAMO=CHAMPIONZ LIGI:

KUNDI A.

1 Esperance Mechi 2 Pointi 6''' Imeingia Nusu Fainali

2 Sunshine Stars Mechi 3 Pointi 6 '' Imeingia Nusu Fainali

3 ASO Chlef Mechi 3 Pointi 0

FAHAMU: ES Sahel ya Tunisia imeondolewa kwenye Mashindano na CAF.

KUNDI B.

1 Al Ahly  Mechi 4 Pointi 10

2 TP Mazembe Mechi 4 Pointi 7

3 Bechem Chelsea Mechi 5 Ponti 6

4 Al Zamalek Mechi 5 Pointi 1

FAHAMU: Timu mbili za juu zinaingia Nusu Fainali.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad