Miradi 10 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 600 kupitiwa na mbio za mwenge wa Uhuru septemba 7 wilayani Ngara mkoani Kagera . - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, September 05, 2012

Miradi 10 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 600 kupitiwa na mbio za mwenge wa Uhuru septemba 7 wilayani Ngara mkoani Kagera .


Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa mwaka 2012 Kapt Honest Ernest Mwanossa akitamka ‘’ Sisi tumekwisha uwasha Mwenge na kuuweka mlima Kilimanjaro,’’baada ya kuwasha Mwenge uliopo Mwitongo Nyumbani kwa Baba wa taifa hayati Mwl Julius K Nyerere.


Na Shaaban Ndyamukama Ngara.



Miradi 10 yenye thamani ya shilingi milioni 635 laki 8 na 17,000 katika Halmashauri ya wilaya ya Ngara mkoani Kagera inatarajiwa kupitiwa na mbio za mwenge utakaowasili septemba 7 wilayani humo .


Akiongea na waandishi  wa habari ofisini kwake jumatatu wiki hii Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Ngara  Simon Mumbee amesema  kamati ya mwenge ya mkoani Kagera ilipitisha miradi hiyo 10 kati ya miradi 14  iliyokuwa imependekezwa  na kamati ya mwenge  wilayani Ngara .


Mumbee alisema kuwa miradi hiyo itafunguliwa ,kukaguliwa ,kuzinduliwa na kuwekewa mawe ya msigi katika  kata za Rusumo , kasulo, Rulenge Keza na  mwenge utakesha katika kata ya Murusagamba na kesho yake  utakabidhiwakatika  kijiji cha Nyabibuye  wilaya mpya  ya Kakonko mkoani Kigoma.


Alisema kuwa katika miradi hiyo serikali kuu ilichangia shilingi zaidi ya milioni 400  wananchi walichangia shilingi milioni 150 na fedha nyingine ilichangiwa na Halmashauri pamoja na wahisani mbalimbali wilayani humo.


Wakimbiza Mwenge kitaifa na baadhi ya makamanda wa jeshi la polisi wakishuka baada ya kuwasha mwenge wa Mwitongo.


Naye martibu wa mbio za mwenge wilayani Ngara Bakari Salumu alisema mwenge utaweka  jiwe la msingi katika ujenzi wa shule ya sekondari Rusumo Maporomoko, mradi wa maji Kafua kata ya Kasulo,  ujenzi wa kituo cha polisi cha kata ya keza   na mradi wa barara ya Murubanga hadi Mursagamba kuelekea mpakani na nchi jirani ya Burundi.


Bakari alisema katika pia mwenge utafungua mradi wa eneo la mnada lililoko Benako, kufungua josho la mifugo Kumubuga kata ya Rusumo na ujenzi wa Zahanati ya Magamba .


Aidha alisema kuwa katika uzinduzi mwenge utazindua bwalo la shule ya sekondari ya RHEC Rulenge na kukagua shamba la miti la mtu binafsi kata ya Murusagamba ambapo aliwataka wananchi kujitokeza kuupokea mwenge huo ulio na kauli mbiu ya shiriki sensa , toa maoni katika mchakato wa katiba mpya na jihadhari na VVU pamoja na kupinga vikali vitendo vya rushwa.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad