![]() |
| Felix Sunzu |
Kampuni
ya Simu za Mkononi ya Vodacom imeingia mkataba wa miaka mitatu na Shirikisho la
Soka Tanzania (TFF) wa kudhamini ligi hiyo ikiwa imepanga kutumia kiasi cha Sh
1.7 bilioni.
Mshindi
wa pili wa ligi hiyo atajizolea, Sh 50 milioni wakati Sh 30 milioni zitakwenda
kwa mshindi wa tatu.
Sunzu
analipwa Dola 3,500 kwa mwezi ambazo ni sawa na Sh 5.4 milioni ambazo
ukizidisha kwa miezi 12 anapata Sh 65.1 milioni na ukiongeza na posho za mechi
na gharama ndogondogo ambazo klabu inaingia, zinazidi Sh 70 milioni za bingwa
wa ligi.
Klabu
zimekuwa zikilalamikia ufinyu wa zawadi huku TFF ikitangaza kwamba mkataba mpya
na mdhamini umeshasainiwa ingawa hakuna picha zozote za ushahidi zilizoonyesha
wahusika wakianguka wino.
Ligi
Kuu inashirikisha timu 14 ambazo zitacheza mechi 26 kuzunguka mikoa mbalimbali
kila timu ikiwa na usajili wa wachezaji wasiopungua 25.
Huku
udhamini wa Tanzania ukiwa kiduchu huko Afrika Kusini ambako kampuni za huko
zimewekeza Tanzania katika sekta za madini, fedha na mawasiliano zinatoa zawadi
za kufa mtu.
Mathalan
bingwa wa Ligi Kuu Afrika Kusini inayodhaminiwa na Benki ya ABSA, ambayo ina
hisa kubwa katika Benki ya Biashara ya Tanzania (NBC), bingwa anaondoka na
kiasi cha Sh 1.9 bilioni.
Mshindi
wa pili wa ligi hiyo anaondoka na kiasi cha Sh 926 milioni huku mshindi wa tatu
akiweka kibindoni Sh 370 milioni.
Kinachoshangaza
ni kuwa kampuni za kigeni zilizowekeza nchini zinamwaga mamilioni huko makwao
lakini linapokuja suala la kudhamini michezo ya Tanzania, zinatoa zawadi ndogo
wakati wanafaidi rasilimali mbalimbali kupitia uwekezaji wao.
imeandikwa
na:http://www.mwanaspoti.co.tz.







No comments:
Post a Comment