Amesema
hayo leo, wakati akiongea na mwandishi wa habari ofisini kwake aliyetaka kujua
fursa za ajira zilizoko na taratibu za mchakato wa ajira tangu kutolewa kwa
tangazo hadi kupangiwa kituo cha kazi.
Daudi
amesema, kwa mfano mwananchi yeyote akitembelea katika tovuti ya Sekretarieti
ya Ajira hivi sasa ataona tangazo la kuitwa kazini kwa waombaji kazi waliofaulu
katika usaili uliofanyika mwezi Juni, 2012 ambao wanatakiwa kuripoti kwa
Waajiri; Wakala wa Vipimo, pamoja na kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na
Utalii.
Mbali na
hilo, pia watakuta tangazo la kuitwa kwenye usaili kwa wale waliokidhi vigezo
kulingana na nafasi walizokuwa wameomba kama zilivyokuwa zimetangazwa kwa niaba
ya Halmashauri ya Wilaya ya Babati, Chuo cha Mipango Dodoma, Taasisi ya Sanaa
na Utamaduni Bagamoyo, Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo na taasisi
nyinginezo.
Aliongeza
kuwa katika Tovuti hiyo watakuta pia tangazo la nafasi za kazi 194 zikiwemo
nafasi za Wakurugenzi, Wakufunzi Waandamizi wa Vyuo, Wakufunzi Wasaidizi,
Wahandisi, Mafundi Sanifu, Wakaguzi wa ndani wa hesabu, Makatibu Mahsusi,
Walinzi, Wapishi na kada nyinginezo.
Aidha,
amesisitiza ni muhimu kwa waombaji kuzingatia masharti ya tangazo pindi
wanapotuma maombi yao kwa njia ya posta ili kujiweka katika nafasi nzuri ya
kupata fursa ya ajira serikalini maana mchakato wa ajira hufuata Sera, Sheria,
Kanuni na Taratibu.
Katibu wa
Sekretarieti ya Ajira alimaliza mahojiano yake kwa kuitaja tovuti ya
Sekretarieti ya Ajira kuwa ni www.ajira.go.tz kwa wale wasioifahamu ili waweze
kuifahamu.
No comments:
Post a Comment