Jose Mourinho asema Cristiano Ronaldo ndiye anayestahili kushinda Ballon d'Or na si Lionel Messi wa FC Barcelona. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, August 04, 2012

Jose Mourinho asema Cristiano Ronaldo ndiye anayestahili kushinda Ballon d'Or na si Lionel Messi wa FC Barcelona.


Meneja wa Real Madrid Jose Mourinho amesema kuwa Mchezaji wake Cristiano Ronaldo ndie anastahili kushinda Ballon d'Or na si Mchezaji wa FC Barcelona Lionel Messi.


Aidha Tuzo ya FIFA Ballon d'Or, au ‘Mpira wa Dhahabu’ huzawadiwa kwa Mchezaji Bora Duniani kwa Msimu uliopita na Tuzo hii ilianzishwa Mwaka 2010 na huendeshwa na FIFA pamoja na Gazeti la Ufaransa la Soka liitwalo ‘France Football’ kufuatia kuunganishwa Tuzo ya FIFA ya Mchezaji Bora Duniani, iliyokuwa ikiendeshwa na FIFA na Ballon d’Or, iliyokuwa ya France Football.


Mshindi wa Tuzo hiyo huchaguliwa na Jopo mchanganyiko la Waandishi wa Habari wa Kimataifa na Makocha wa Timu za Taifa na Makepteni wao.


Mchezaji Lionel Messi wa FC Barcelona ndie alietwaa Tuzo hii ilipoanzishwa kwa mara ya kwanza hapo Mwaka 2010 na pia alitwaa Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani Mwaka 2009.


Cristiano Ronaldo, ambae sasa ni Mchezaji wa Real Madrid, alishinda Tuzo hiyo Mwaka 2008 wakati akiwa na Manchester United.


Kocha Mourinho alisema: “Kwangu mimi, Mchezaji Bora wa Msimu ndie anaeshinda Taji hilo.” Aliongeza: “Ronaldo ameisaidia Timu kushinda kitu kikubwa na sidhani katika historia ya Ballon d'Or Mchezaji anatwaa Tuzo bila kushinda kitu kikubwa. Sasa sidhani Messi bila kushinda CHAMPIONZ LIGI, bila kushinda La Liga, atatwaa Ballon d'Or.”


Msimu uliopita, Ronaldo alifunga bao 46 kwenye La Liga na kuiwezesha Real Madrid kutwaa Ubingwa baada ya kuukosa kwa Miaka minne lakini Messi alikuwa ndie Mfungaji Bora akiwa na bao 50 huku Barcelona yake ikimaliza nafasi ya pili na Mwezi Januari Mwaka huu alitwaa Taji la Ballon d'Or kwa mara ya 3 mfululizo.


Mshindi wa Mwaka 2012 atatangazwa Januari Mwakani.


WASHINDI WA ZAMANI WA BALLON D'OR:

1956 Stanley Matthews

1957 Alfredo Di Stefano

1958 Raymond Kopa

1959 Alfredo Di Stefano

1960 Luis Suarez

1961 Omar Sivori

1962 Josef Masopust

1963 Lev Yashin

1964 Denis Law

1965 Eusebio

1966 Bobby Charlton

1967 Florian Albert

1968 George Best

1969 Gianni Rivera

1970 Gerd Mueller

1971 Johan Cruyff

1972 Franz Beckenbauer

1973 Johan Cruyff

1974 Johan Cruyff

1975 Oleg Blokhin

1976 Franz Beckenbauer

1977 Allan Simonsen

1978 Kevin Keegan

1979 Kevin Keegan

1980 Karl-Heinz Rummenigge

1981 Karl-Heinz Rummenigge

1982 Paolo Rossi

1983 Michel Platini

1984 Michel Platini

1985 Michel Platini

1986 Igor Belanov

1987 Ruud Gullit

1988 Marco van Basten

1989 Marco van Basten

1990 Lothar Matthaeus

1991 Jean-Pierre Papin

1992 Marco van Basten

1993 Roberto Baggio

1994 Hristo Stoichkov

1995 George Weah

1996 Matthias Sammer

1997 Ronaldo

1998 Zinedine Zidane

1999 Rivaldo

2000 Luis Figo

2001 Michael Owen

2002 Ronaldo

2003 Pavel Nedved

2004 Andriy Shevchenko

2005 Ronaldinho

2006 Fabio Cannavaro

2007 Kaka

2008 Cristiano Ronaldo

2009 Lionel Messi

2010 Lionel Messi

2011 Lionel Messi      

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad