Robin van Persie na Shinji Kagawa wawapa furaha Manchester United huku Torres na Hazard wakiipeleka Chelsea kileleni mwa Ligi kuu soka Uingereza. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, August 26, 2012

Robin van Persie na Shinji Kagawa wawapa furaha Manchester United huku Torres na Hazard wakiipeleka Chelsea kileleni mwa Ligi kuu soka Uingereza.


Robin van Persi
Kufuatia kipigo cha Mechi ya kwanza, Manchester United katika Mechi yake ya kwanza Uwanja wa nyumbani wa Old Trafford na Straika  na Robin van Persie alieanzishwa na kocha Sir Alex Ferguson  hakufanya makosa alipofunga bao lake la kwanza na la kusawazisha huku mchezaji Shinji Kagawa akipiga bao la pili na kuisaidia Manchester United kuifunga Fulham kwa bao 3-2 katika Ligi kuu soka nchini Uingereza hapo jana Jumamosi.


Man United walianza vibaya katika Mechi hii pale udhaifu wa Difensi yao , ambayo Kiungo Michael Carrick kwa mara ya pili akicheza kama Sentahafu, ilipofanya makosa na kuwapa Fulham bao la kwanza katika Dakika ya 3 tu.


Lakini bao za Robin van Persi, Shinji Kagawa na Rafael ziliwafanya Man United wawe mbele kwa bao 3-1 hadi mapumziko.


Udhaifu wa Difensi ya Man United uliwapa zawadi bao la pili Fulham pale Vidic na Kipa De Gea walipocheza ovyo na Vidic kujifunga mwenyewe.

Sir Alex Ferguson amesema Robin van Persie atazidi kuwa bora kadri muda unavyokwenda na amemsifia kwa kufunga bao lake la kwanza kwa Klabu yake Manchester United ambalo aliliita bao zuri sana lakini akatoboa kuwa Wayne Rooney atalazamika kukaa nje ya Uwanja kwa Wiki 4 baada ya kuchanika pajani.



Chelsea

Nao Mabingwa wa Ulaya  Chelsea wakicheza  Mechi yao ya  tatu za Ligi Kuu Uingereza, kila Mechi wakipata na kufunga Penati, sasa wameshinda Mechi zote hizo tatu na wako kileleni, ambapo wakicheza kwao Stamford Bridge wameichapa Newcastle bao 2-0.


Chelsea walipata bao lao la kwanza katika Dakika ya 22 kwa Penati iliyopigwa na Mchezaji wao mpya Eden Hazard na bao lao la pili katika Dakika ya 45 kwa bao la Fernando Torres baada ya kutengenezewa na Eden Hazard.


Mechi inayofuata kwa Chelsea ni huko Monaco hapo Agosti 31 kugombea UEFA Super Cup dhidi ya Atletico Madrid ambao ni Mabingwa wa EUROPA LIGI.


Brendan Rodgers
Ligi hiyo soka Uingereza inaendelea tena leo Jumapili Agust 26 kwa Liverpool, wakiwa kwao Anfield, wana kibarua kigumu dhidi ya Mabingwa watetezi Manchester City.


Liverpool wako kwao Anfield na watataka ushindi baada ya kutwangwa 3-0katika Mechi yao ya kwanza ya Ligi mikononi mwa WBA lakini, hata hivyo, watamkosa Sentahafu wao Daniel Agger ambae alitolewa kwa Kadi Nyekundu katika kipigo hicho Wikiendi iliyopita.


Nasri na Toure
Man City, ambao waliifunga kwa taabu Southampton, hawajawahi kushinda Anfield tangu Mwaka 2003 na wataingia kwenye Mechi hii bila wa Straika wao mkubwa Sergio Aguero ambae aliumia goti Wikiendi iliyopita na hivyo itawabidi wachague nani wa kucheza pamoja na Straika Carlos Tevez kati ya Edin Dzeko na Mario Balotelli.



Arsene Wenger
Aidha Stoke City  watapambana na  Arsenal ambapo timu hizi zote zilitoka sare katika Mechi zao za kwanza na Arsenal wameshinda Mechi moja tu kati ya 4 walizocheza mwisho kwenye Uwanja wa Britannia.


Stoke wanategemewa kumuanzisha Mchezaji mpya Geoff Cameron ambae atacheza Kiungo pamoja na Glenn Whelan huku Jonathan Walters akicheza nyuma tu ya Straika Peter Crouch.


Lukas Podolski

Kwa Arsenal, Santi Cazorla, Mikel Arteta na Abou Diaby wataendelea kucheza Kiungo baada ya kucheza vizuri katika sare na Sunderland huku Fowadi ikikamatwa tena na Gervinho na Lukas Podolski.
Arsenal wana nafasi nzuri kushinda Mechi hii lakini inabidi waidhibiti nguvu kazi ya Stoke City.







Aidha kwa Matokeo na ratiba za Ligi nyingine unaweza tazama LIVE kwenye Blogg hii kwa juu.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad