Msanii Roma apata ajali na gari lake akielekea mkoani Morogoro kwenye show. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, August 04, 2012

Msanii Roma apata ajali na gari lake akielekea mkoani Morogoro kwenye show.

Muda mchache uliopita msanii wa kizazi kipya kwenye bongo hip hop ROMA amepata ajali mbaya barabara ya Morogoro. 


Roma anasema alikuwa yupo kwenye mwendo wa kawaida ndio tairi la mbele lilipopata pancha na ndipo gari likaacha njia yake na kwenda kugongana uso kwa uso na fuso ambalo lilikuwa upande wa pili na gari hilo dogo alilokuwa akiendesha Roma kurudi lilipotokea.


Roma ananiambia kwa sasa anaelekea Hospital kwa check up zaidi ila aliokuwa nao kwenye gari hakuna aliyeumia wote ni wazima.




Huyu ni mmoja kati ya marafiki wa Roma aliyekuwa nae kwenye gari wakielekea Morogoro kwenye show


Roma akimwelezea police wa usalama barabarani kilichotokea mpaka kupata ajali hiyo mbaya.

 
Source DJ CHOKA.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad