![]() |
Rais wa CWT-
Bw.Gratian Mukoba.
|
Chama Cha
Walimu Tanzania-CWT-kimetangaza kusitisha rasmi mgomo wa walimu na hivyo
kuwataka walimu wote nchini kurejea kazini mara moja kuanzia leo ili kutekeleza
majukumu yao ya kila siku kama kawaida.
Akitoa tamko
la CWT kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku moja
baada ya Mahakama Kuu Kitengo cha Kazi kukiagiza Chama hicho kitoe maelekezo
kwa wanachama wake kurudi kazini, Rais wa Chama hicho Gratian Mukoba amesema
walimu wanarudi kazini wakiwa wamekata tamaa kutokana na hukumu hiyo.
Amefafanua
kuwa walimu wanaporudi kazini bila kuwa na mawazo yaliyotulia, utendaji wao
utaathirika hivyo Chama kinatoa wito kwa Serikali kukutana na CWT kwa haraka
ili kuendeleza majadiliano ya Madai mapya ya Walimu.
Kuhusu
kulipa fidia ya hasara waliyoipata wanafunzi, Chama hicho kimesema kinasubiri
taarifa rasmi ya Serikali kuhusu hasara hiyo kwa kuwa hakina uwezo wa kufahamu
hasara waliyoipata wanafunzi.
Kwa mujibu
wa Mukoba wenye uwezo wa kuwasilisha hasara hiyo ni mlalamikaji katika kesi
hiyo ambaye ni Serikali.
Hapo jana
Chama hicho kilipongeza kauli ya Rais Jakaya Kikwete alisema Serikali inajali
na kuthamini mchango wa Walimu nchini.
Sorce:wegambanews.blogspot.com
No comments:
Post a Comment