Hawa ndio viongozi wa timu ya Walimu FC ya wilayani Ngara mkoani Kagera. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, August 04, 2012

Hawa ndio viongozi wa timu ya Walimu FC ya wilayani Ngara mkoani Kagera.

Kikosi cha timu ya Walimu FC.

Klabu ya Walimu FC ya wilayani Ngara mkoani Kagera hii leo (August 3 ) mwaka huu imefanya uchaguzi wa kuchagua viongozi watakao iongoza klabu hiyo, katika nafasi  za Mwenyekiti,Makamu mwenyekiti,Katibu mkuu,Katibu msaidizi,Mweka hazina pamoja na katibu mwenezi.



Kwa mujibu wa msimamizi wa uchaguzi huo kutoka chama cha soka wilaya ya Ngara mkoani Kagera NDFA Seif Omary Upupu aliyechaguliwa katika nafasi ya Mwenyekiti ni Supery Jeremiah kwa kupata kura 13 ili hali Makamu wake ni Hezron Kayanda kwa kura 14.



Kwa  upande wa katibu mkuu ni Faustine Malulu aliyechaguliwa kwa kura 16 huku msaidizi wake ni Vedastus Gunda kura 14 pamoja na Denice Mutasigwa kura 2.


Waliochaguliwa katika nafasi ya mweka hazina ni pamoja na Rosemary Pastory kura 14 na Neema Rujuba kura 0 huku Katibu mwenezi akichaguliwa  Godfrey Cyprian kura 16.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad