Mchezaji Mrisho Ngassa aanza rasimi mazoezi na klabu yake ya Wekundu wa Msimbazi Simba. - Mwana Wa Makonda
cV7ufzj

Muhtasari

X-BET

MAIN-

Post Top Ad

cV7ufzj

Friday, August 03, 2012

demo-image

Mchezaji Mrisho Ngassa aanza rasimi mazoezi na klabu yake ya Wekundu wa Msimbazi Simba.

.com/simgad/

8

Kama kawa na jezi yake ile ile namba 16

Hapo Jana Club ya soka ya Azam ilitangaza kwamba Mchezaji wao Mrisho Ngasa tayari amepelekwa Simba kwa mkopo ambapo Simba walipewa sharti la kuhakikisha wanamlipa Ngasa mshahara wake kamili (TZsh 2,000,000) kwa mwezi pamoja na stahiki zake nyingine zote za kimkataba.


Sababu za kumpeleka Ngasa kwa mkopo ni kumuepusha na adhabu ambayo klabu ya Azam FC ingetoa kwa Ngasa kama angebaki Azam Fc, Pia iliwekwa wazi kwamba Azam haijamlazimisha Ngasa kwenda Simba kama inavyopotoshwa, Kama Ngasa anataka kuvunja mkataba wake au kama Yanga bado wanamhitaji basi waje na dola 50,000 na Azam FC itawauzia kwani licha ya kwamba amepelekwa kwa mkopo simba lakini Ngasa bado ni mali ya Azam FC.

 

52

Ngassa akipambana na Amri Kiemba


 

Azam ilisema “Tunaomba kuweka msimamo wetu kuwa hatupo tayari kumlipa Ngasa na kuvunja mkataba wake na hatuna sababu ya kufanya hivyo. Kama Ngasa hataki kwenda tunakompeleka Azam FC inamruhusu kubakia klabuni na kutumikia adhabu, Lakini Ngasa na washauri wake waelewe kuwa akiamua kubaki Azam FC atakaa nje ya uwanja kwa muda wote uliosalia kwenye mkataba wake, kwani Azam FC haipotayari kumvisha jezi mchezaji anayefanya vitendo vya utovu wa nidhamu”

 

395790_336743119748157_806937205_n

Aliyekuwa mchezaji wa Azam,Mrisho Ngassa akiwa ameegemea gari yake aliyokabidhiwa jana mara baada ya kuwasili katika ufukwe wa Coco Beach kwa kuungana na wachezaji wenzake wa Simba baada ya maridhiano ya Azam,Simba na yeye kumalizika

 

Azam ilisema kosa alilolifanya Ngasa ni kubusu na kuvaa jezi ya Yanga wakati bado ni mchezaji wa Azam hivyo ilionekana ni kitendo cha nidhamu mbovu na kuidhalilisha brand ya Azam.

 

42

 

83

Jinsi Mrisho Ngasa alivyopokewa na mashabiki wa Simba kwenye makao makuu ya klabu hiyo.

13-800x533

Hili ndio gari jipya la Mrisho Ngasa alilopewa kwenye huo uhamisho wa kuingia Simba kwa mkopo akiwa anaingia nalo kwenye mazoezi na Simba .

 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Contact Form

Name

Email *

Message *