Liverpool, Inter & Athletic Bilbao ZASHINDA EUROPA LIGI - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, August 03, 2012

Liverpool, Inter & Athletic Bilbao ZASHINDA EUROPA LIGI

Hapo jana usiku kwenye Mechi za Raundi ya Tatu ya Mtoano ya EUROPA LIGI Klabu Vigogo, Liverpool, Inter Milan na Timu iliyofungwa kwenye Fainali ya Kombe hili Mwezi Mei Athletic Bilbao, zote zilianza vyema katika Mechi zao za kwanza kwa Liverpool kushinda ‘kiduchu’ ugenini huko Belarus huku Inter Milan ikitwanga 3-0 ugenini huko Croatia na Bilbao kushinda nyumbani bao 3-1.

Liverpool iliifunga FC Gomel bao 1-0 ugenini kwa bao la Dakika ya 68 la Stewart Downing.

Inter Milan wao waliichapa Klabu ya Croatia HNK Hajduk Split bao 3-0 kwa bao za Wesley Sneider, Yuto Nagatomo na Philippe Coutinho.




Nao Athletic Bilbao, waliocheza nyumbani, waliifunga Klabu nyingine kutoka Croatia NK Slaven Koprivnica bao 3-1 kwa bao za David Lopez, bao mbili, na Markel Susaeta Laskurain na bao la NK Slaven Koprivnica lilifungwa na Delic.

Marudiano ya Raundi ya Tatu ya Mtoano ni Agosti 9.

YAFUATAYO NI MATOKEO YA MECHI ZOTE 29:

RAUNDI YA TATU YA MTOANO:

MATOKEO Mechi za Kwanza:

Alhamisi Agosti 2

FC Anzhi -  2 Vitesse Arnhem -  0

DILA Gori - 0 Anorthosis Famagusta FC –  1

Apoel Nicosia -  2 Aalesunds FK –  1

Ried -  2 Legia Warsaw -  1

Tromso - 1 FC Metalurg Donetsk -  1

 Ruch Chorzow SA - 0 FC Viktoria Plzen -  2

 Horsens -  1 Elfsborg –  1

 Bnei Yehuda -  0 PAOK FC –  2

 FC Twente Enschede -  2 Mlada Boleslav -  0

 Servette -  1 Rosenborg BK –  1

 KRC Genk - 2 Aktobe -  1

 FC Steaua Bucuresti -  0 Trnava –  1

 FC Gomel -  0 Liverpool –  1

 Asteras Tripolis FC -  1 Maritimo –  1

 St Patrick -  0 Hannover 96 –  3

 Athletic de Bilbao -  3 NK Slaven Belupo –  1

 Vojvodina - 2 SK Rapid Wien –  1

 HNK Hajduk Split –  0 Inter Milan -  3

 Videoton Szekesfehervar -  1 KAA Gent –  0

 Dundee United FC - 2 Dinamo Moscow -  2

 AIK Solna - 3 KKS Lech Poznan -  0

 FK Sarajevo -  2 Zeta – 1

 SC Heerenveen –  4 FC Rapid Bucuresti –  0

 KuPS - 1 Bursa Bursaspor –  0

 Arsenal Kyiv - 3 Mura –  0

 Kalmar -  1 BSC Young Boys –  0

 FK Crvena zvezda -  0 Omonia Nicosia FC –  0

 EskiÅŸehirspor - 1 Olympique de Marseille -  1

 Trenkwalder Admira - 0 AC Sparta Prague -  2

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad