![]() |
Mwanafunzi anapoamua kuchukua nafasi ya ualimu. Hakika hapa ndipo inapoonekana walimu ni watu/walezi muhimu sana. |
Mahakama kuu divisheni kazi leo imebatilisha mgomo wa walimu nchini uliokuwa ukiendelea kwa lengo la kushinikiza serikali ili kuboresha masilahi yao.
Hatua hiyo imekuja baada ya serikali kufungua kesi mahakamani ikitaka mgomo huo ubatilishwe.
Makama kuu divisheni ya kazi imesema mgomo ulioitishwa na chama cha walimu CWT haukuwa halali hivyo kuamuru walimu wote kurejea kazini.
Kufuatia tamko hilo la mahakama katibu wa chama cha walimu wilaya ya Ngara mkoani Kagera Bw Vedastus Nsinde akawataka walimu wote wilayani Ngara kesho August 3, 2012 kuendelea na kazi kama kawaida wakati taratibu nyingine zikiendelea.
Tangu July 30 mwaka huu walimu waligoma wakishiniki serikali kuboresha masilahi na mazingira bora ya kazi.
![]() |
Walimu wamegome je sisi wanafunzi tufanyeje?? Kumbukeni kuwa sisi tuna haki ya kupata ELIMU. |
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na wahariri Ikulu jana. |
No comments:
Post a Comment