Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akihojiwa na Karani wa
sensa Beatrice Nchimbi wakati
alipojiandikisha kijini kwake Kibaoni, mkoani Katavi, Agust 26,2012.(Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu).
Aidha Waziri mkuu Mizengo Pinda amesema posho kwa
ajili ya wenyeviti wa vitongoji na vijiji ambao wataambatana na makarani wa
sensa zipo palepale na kwamba hawana haja ya kuhofu juu ya malipo yao.
Waziri Mkuu ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya
Kitaifa ya Sensa amewasihi wenyeviti hao waendelee na kazi yao bila wasiwasi
wowote kwani watalipwa.
“Ni kweli malipo yao yamechelewa, ni suala la
wikiendi tu kuingilia hapa kati, lakini napenda niwahakikishie kwamba stahili
zao zipo, wao wachape kazi tu!” alisisitiza.
Alisema ameona kwenye taarifa za habari kupitia
baadhi ya luninga wakidai kwamba wameachwa katika malipo ya kazi hiyo lakini
akatumia fursa hiyo kuwahakikishia kwamba watalipwa. “Nimeona kwenye TV wanadai
kuwa wameachwa, si kweli. Nawahakikishia wote kwamba wako katika hesabu yetu na
wote watalipwa,” aliongeza.
Pia Waziri
Mkuu Pinda aliwaomba Watanzania watambue kuwa zoezi hili lilianza tangu mwaka
2004 na lina gharama kubwa kwani mpaka sasa limegharimu zaidi ya sh. bilioni
140/-.
Alisema ukweli huo unabainishwa na maswali yaliyomo
kwenye dodoso la sensa ambayo yanalenga kujua jinsi za watu, umri wao, shughuli
zao za kiuchumi na kuwaweka katika makundi ili iwe rahisi kuwahudumia.
Aliwasihi Watanzania ambao hawatahesabiwa leo kuwa
wavumilivu kwani zoezi hilo litaendelea kwa muda wa siku saba. “Makarani
wataendelea kutembelea kaya kwa siku saba zijazo, cha msingi mkuu wa kaya
aandae taarifa za watu waliolala kwenye mji wake usiku wa tarehe 25 kuamkia
tarehe 26 Agosti, mwaka huu. Aorodheshe majina yao, umri wao, elimu yao, jinsi
zao na shughuli ambazo wanazifanya,” alifafanua.
Kuhusu watu wanaopinga sensa, Waziri Mkuu alisema
anaunga mkono kauli zilizotolewa na Rais Jakaya Kikwete pamoja na Rais wa
Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein la kuwataka Watanzania wote washiriki zoezi la
sensa.
|
No comments:
Post a Comment