Jopo
la mahakama moja ya Marekani limeamua kuwa kampuni kubwa ya teknolojia ya Korea
Kusini, Samsung, iliiga baadhi ya ufundi mpya wa kampuni ya Marekani ya Apple
kuunda simu zake wenyewe za kisasa za smartphone na kumputa ndogo - tablet.
![]() |
|
Simu
za Apple na Samsung
|
Baada
ya kesi iliyoendelea kwa mwaka mzima, ambayo ilichunguza mashtaka kama 700 ya
aina ya ufundi ulioigwa, mahakama ya California yaliiamrisha Samsung iilipe
Apple fidia ya dola zaidi ya bilioni moja.
Samsung
imelalamika kuwa Apple inajaribu kuhodhi soko zima la smartphone, na imesema
itakata rufaa.
Zaidi
ya nusu ya simu za smartphone zinazouzwa duniani ni ama za Apple au Samsung, na
kampuni hizo mbili zinashtakiana katika mahakama ya nchi mbali mbali duniani.






No comments:
Post a Comment