Wilaya ya kibondo mkoani kigoma inakabiliwa na uharibifu mkubwa wa mazingira . - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, July 05, 2012

Wilaya ya kibondo mkoani kigoma inakabiliwa na uharibifu mkubwa wa mazingira .

(Misitu ni Mali)

Wilaya ya kibondo mkoani kigoma inakabiliwa na uharibifu mkubwa wa mazingira kutokana na kuongezeka kwa vitendo vya uchomaji misitu na kilimo katika vyanzo vya maji .

Afisa mazingira wilayani kibondo Bw Mohamed Semdoe amesema kuwa idara ya mazingira imekusudia kuanzisha kamati ndogo za kuhifadhi mazingira katika vijiji mbalimbali wilayani humo .

(Mzinga wa nyuki katika Misitu  yetu)



Bw Semdoe amekiri kuwa wilaya ya Kibondo inakabiliwa na changamoto kubwa katika uharibifu wa mazingira na kwamba athari za uharibifu wa mazingira zimekuwa zikiongezeka kutokana na harakati za binadamu kutaka kujiletea maendeleo kiuchumi, kijamii na kiutamaduni.


Amewataka Wananchi kuzingatia sharia na kanuni za kuhifadhi mazingira kwani bila kujali athari zake  hali inayosababisha kutokea kwa mabadiliko ya tabia nchi na kuhatarisha maisha ya binadamu.

 

Source: Radio Kwizera FM.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad