LISTI ya FIFA UBORA DUNIANI: Hispania juu palepale huku Tanzania yapanda nafasi 12 ipo 127! - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, July 04, 2012

LISTI ya FIFA UBORA DUNIANI: Hispania juu palepale huku Tanzania yapanda nafasi 12 ipo 127!

Tanzania imependa kwa nafasi 12 kwenye orodha ya viwango vya ubora ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) iliyotolewa leo (Julai 4 mwaka huu) na shirikisho hilo.

Kwa viwango vya Juni mwaka huu, Tanzania (Taifa Stars) ambayo timu yake inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ilikuwa namba 139 hivi sasa imefika nafasi ya 127 ikiwa na pointi 253 kulinganisha na 214 za Juni mwaka huu.

Ivory Coast inayoshika nafasi ya 16 duniani bado inaongoza kwa upande wa Afrika ikiwa na pointi 939. Timu hiyo ilikuwa katika nafasi hiyo hiyo kwa viwango vilivyotolewa Juni 6 mwaka huu. Hispania ambao ni mabingwa wa Ulaya na Dunia ndiyo wanaoendelea kuongoza kwa kukamata nafasi ya kwanza wakiwa na pointi 1,691.


Hispania , ambao ndio Mabingwa wa Ulaya na Dunia, wameendelea kushika Nambari Wani kwenye Listi ya FIFA/Coca Cola ya Ubora Duniani iliyotolewa leo huku Tanzania ikipanda nafasi 12 na kushikilia Nambari 127.

Italia, ambao walifungwa na Hispania kwenye Fainali ya EURO 2012 Jumapili iliyopita, wamepanda nafasi 6 na kurudi tena kwenye 10 bora na sasa wako nafasi ya 6 huku Portugal/Ureno wakipanda nafasi 5 na kukamata nafasi ya 5 ili hali Uingereza  wamepanda nafasi mbili na kushika nafasi ya 4.

Listi nyingine itatolewa Agosti 8.

20 BORA:

1 Hispania

2 Ujerumani

3 Uruguay

4 Uingereza

5 Portugal

6 Italia

7 Argentina

8 Uholanzi

9 Croatia

10 Denmark

11 Brazil

12 Greece

13 Russia

14 Ufaransa

15 Chile

16 Côte d'Ivoire

17 Sweden

18 Czech Republic

19 Mexico

20 Japan


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad