Majambazi yavamia familia tano za kijiji cha Igarula kata ya Kachwamba wilayani Chato mkoani Geita na kupora vitu vyenye thamani ya shilingi milioni nane. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, July 13, 2012

Majambazi yavamia familia tano za kijiji cha Igarula kata ya Kachwamba wilayani Chato mkoani Geita na kupora vitu vyenye thamani ya shilingi milioni nane.


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu (kulia) wakikagua jengo la Halmashauri ya wilaya ya Chato baada ya kulifungua wakiwa katika ziara ya mkoa wa Kagera Machi 6, 2011. Wa pili kushoto ni  aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mohamed Babu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Watu wanaosadikika  kuwa majambazi wamezivamia familia tano za kijiji cha Igarula kata ya Kachwamba wilayani Chato mkoani Geita na kupora vitu vyenye thamani ya shilingi milioni nane.

Tukio hilo limetokea majira ya saa nane usiku wa kuamkia leo ambapo Mmoja wa watu waliovamiwa Bw Naftari Anthon amesema kabla ya kupora watu hao walifyatua risasi hewani ili kuwatishia watu wasiweze kutoa msaada.

Amesema baada ya hapo watu hao walianza kupora nyumba hadi nyumba na kuiba shilingi milioni tano pamoja na pikipiki mbili.

Amesema watu hao waliondoka na pikipiki hizo na walipofika katika kijiji cha Mwangaza pikipiki moja ilipata pancha na hivyo kuitelekeza kabla ya kuzingirwa na kundi la wananchi katika kijiji cha Kawimiyole na kuwalazimu kuitelekeza na pikipiki ya pili na kisha kukimbia.

Jeshi la polisi wilayani Biharamulo limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba uchunguzi unaendelea.

Aidha Wilaya ya Chato ni wilaya mojawapo ya Mkoa wa Geita. 

Katika sensa ya mwaka 2002, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 251,261 [1] na imekadiriwa kuwa na 318,000 kwa mwaka 2007.

Wilaya hii ilianzishwa mwaka 2007 kutokana na maeneo ya wilaya ya Biharamulo, mkoa wa Kagera, halafu mwaka 2012 ikasogezwa katika mkoa mpya wa Geita.

 

Source:Radio Kwizera.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad