Atletico yaanza michuano ya kagame kwa kuichapa Yanga bao 2-0 Taifa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, July 14, 2012

Atletico yaanza michuano ya kagame kwa kuichapa Yanga bao 2-0 Taifa.

Klabu ya soka ya Yanga ya jijini Dar es salaam ambao ndio mabingwa watetezi wa michuano ya Ubingwa wa Klabu wa Afrika Mashariki na Kati, Kagame Cup,  wanaanza vibaya michuano hii kwa kufungwa mabao 2-0.

Mchezo huo uliopigwa kwenye  Uwanja wa Taifa Mjini Dar es Salaam ikiwa ni  Mechi mbili  za ufunguzi za Kundi C , Atletico ya Burundi walionekana kumiliki sana mpira kuliko Yanga, na nafasi kadhaa walizotengeneza wamefanikiwa kuzitumia vizuri mbili na kupeleka kupata ushindi huu.


Mashindano ya Mwaka huu yanashirikisha Vilabu 11 ambavyo vyote vimeripotiwa na TFF kuwa vimeshaingia Jijini Dar es Salaam na kupangiwa Hoteli mbali mbali.

Timu hizo 11 zimepangwa katika Makundi matatu yatakayocheza Mtindo wa Ligi na Timu tatu tatu, kutoka Kundi A na C yenye Timu 4 kila moja, na Timu mbili toka Kundi B, lenye Timu 3, ndizo zitaingia Robo Fainali itayochezwa kuanzia Julai 23.



KUNDI A
Timu 3 kwenda Robo Fainali.

Simba
URA [Uganda]
Vita [Congo DR]
Ports [Djibouti]

KUNDI B
Timu 2 kwenda Robo Fainali.

Azam FC
Mafunzo [Zanzibar]
Tusker [Kenya]

KUNDI C
Timu 3 kwenda Robo Fainali.

Yanga
APR  [Rwanda]
Wau Salaam [Sudan Kusini]
Atletico [Burundi]

RATIBA:
Julai 14 Jumamosi

1  APR vs WAU SALAAM [Uwanja wa Taifa, Saa 8 Mchana]
2 YANGA 0 vs  2 ATLETICO SALAAM [Uwanja wa Taifa, Saa 10 Jioni]

Julai 15 Jumapili

3 AZAM vs MAFUNZO  [Chamazi Saa 10 Jioni]
4 VITA CLUB vs PORTS [Chamazi, Saa 8 Mchana]
5 SIMBA vs URA  [Uwanja wa Taifa, Saa 10 Jioni]

Julai 17 Jumanne

6 ATLETICO vs APR [Uwanja wa Taifa, Saa 8 Mchana]
7 WAU SALAAM vs YANGA [Uwanja wa Taifa, Saa 10 Jioni]

Jumatano Julai 18

8 VITA CLUB vs URA [Uwanja wa Taifa, Saa 8 Mchana]
9 PORTS vs SIMBA [Uwanja wa Taifa, Saa 10 Jioni]

Julai 19 Alhamisi

10 ATLETICO vs WAU SALAAM  [Uwanja wa Taifa, Saa 8 Mchana]
11 MAFUNZO vs TUSKER [Uwanja wa Taifa, Saa 10 Jioni]

Julai 20 Ijumaa

12 PORTS vs URA  [Uwanja wa Taifa, Saa 8 Mchana]
13 YANGA vs APR  [Uwanja wa Taifa, Saa 10 Jioni]

Julai 21 Jumamosi

14 AZAM vs TUSKER [Uwanja wa Taifa, Saa 8 Mchana]
15 SIMBA vs VITA CLUB [Uwanja wa Taifa, Saa 10 Jioni]

ROBA FAINALI
Julai 23 Jumapili

16 B2 vs C2
17 A1 vs C3

Julai 24 Jumatatu

18 C1 vs A2
19 B1 vs A3

NUSU FAINALI
Julai 26

20 Mshindi 16 vs Mshindi 17
21 Mshindi 18 vs Mshindi 19

Mshindi wa 3:
Julai 28 Jumamosi

Aliefungwa 20 vs Aliefungwa 21

FAINALI:
Julai 28 Jumamosi

23 Mshindi 20 vs Mshindi 21


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad