Kutokana na mkoa wa Kagera kuathirika kwa kiasi kikubwa na Ukataji na Uchomaji Moto Misitu , wafugaji, wakulima na wawindaji Watahadharishwa kujiepusha na vitendo hivyo’’ - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, July 13, 2012

Kutokana na mkoa wa Kagera kuathirika kwa kiasi kikubwa na Ukataji na Uchomaji Moto Misitu , wafugaji, wakulima na wawindaji Watahadharishwa kujiepusha na vitendo hivyo’’

Kutokana na Ukataji na Uchomaji Moto Misitu kukithiri nchini ,Ni vema wadau na jamii kutafuta njia zitakazosaidia kukomesha vitendo vya uchomaji moto misitu nchini.

Mazingira ni kitu cha muhimu sana katika kila jamii duniani na ni kitu ambacho kinahitaji umakini mkubwa, kuanzia ngazi ya familia hadi ngazi ya taifa.

Ni jukumu la kila mmoja wetu kutunza mazingira kwani Uchafuzi wa mazingira unasababisha athari nyingi katika jamii.

Mojawapo ya vyanzo  vya uchafuzi huo wa mazingira ni uchomaji moto ovyo.

Mkuu wa mkoa Kagera  licha ya kusisitiza na kutoa maonyo mbalimbali juu ya uchomaji moto ovyo lakini baadhi ya watu wasio na huruma huamua kuchoma moto kama sehemu hii hapa chini inavyoonekana.

Afisa mazingira wa wilaya ya Ngara mkoani Kagera Bw Mhina Ally Toba amewatahadharisha wafugaji, wakulima na wawindaji kujiepusha na vitendo vya uchomaji moto ovyo katika shughuli zao .

Bw Toba amesema kuwa imekuwa desturi kwa jamii hizo kuchoma moto misitu na mapori mbalimbali hususani wakati wa kiangazi wakijiandaa na shughuli zao ikiwemo kuandaa mashamba, uwinddaji pamoja na kuandaa malisho mapya.

 

Itapendeza sana tukiyatunza mazingira yetu ili yatutunze kama inavyoonekana hapa chini

Amesema serikali haitasita kuwachukulia hatua watakaobainika kuhusika na uchomaji moto ovyo kwa kuwa vitendo hivyo vinaharibu mazingira kwa kiasi kikubwa na kwamba mkoa wa Kagera umeathirika kwa kiasi kikubwa na moto licha ya wananchi kufahamu madhara yatokanayo na moto hasa baada ya kupewa elimu.

Bw Toba pia amewasisitiza viongozi wa vijiji kuhakikisha suala la mazingira linaendelea kuwa ajenda ya kudumu katika vikao vyote vya serikali ya kijiji ili kuhamasisha utunzaji wa mazingira.

Aidha Wizara ya maliasili na utalii imesema kuwa kukithiri kwa vitendo vya ukataji na uchomaji moto misitu nchini hausababishwi na udhaifu wa sheria na sera zinazosimamia misitu nchini kamawadau wengi wanavyofikilia.

Kulingana na Mkurugenzi mkuu wa idara ya  misitu na nyuki nchini Dr. Felician Kilahama amesema tatizo kubwa ambalo limekuwa likiongeza kasi ya ukataji na uchomaji wa misitu katika maeneo mbalimbali ya nchi, ni wananchi kutegemea misitu katika kuendesha maishaya yao  kila siku,kushindwa kuheshimu na kutambua kuwa pasipo misitu hakuna maisha na kukosa uelewa wa faida za misitu.

Aidha mkurugenzi huyo mkuu wa idara ya misitu na nyuki Tanzania amesema kuwa wastani wa hekta laki nne za misitu zimekuwa zikikatwa kila mwaka, huku wastani wa hekta 65,000 zikiteketea kwa motoi kila mwaka, hatua ambayo kama haitadhibitiwa itapelekea nchi kuwa jangwa na kusababisha njaa na ukosefu wa nishati ya umeme.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad