Wananchi wilayani Ngara Mkoani Kagera wamesema kata zilizopangwa kwa ajili ya kutolea maoni ya kuundwa kwa katiba mpya zinaweza kuwa kikwazo kwa wengine kutoshiriki kutoa maoni yao. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, July 04, 2012

Wananchi wilayani Ngara Mkoani Kagera wamesema kata zilizopangwa kwa ajili ya kutolea maoni ya kuundwa kwa katiba mpya zinaweza kuwa kikwazo kwa wengine kutoshiriki kutoa maoni yao.


Baadhi ya wananchi wa wilayani Ngara wamesema kata zilizopangwa kwa ajili ya kutolea maoni ya kuundwa kwa katiba mpya wilayani Ngara mkoani Kagera inaweza kuwa kikwazo kwa wengine kutoshiriki kutoa maoni yao.

Wakizungumza na waandishi wa habari,baadhi ya  wananchi hao wamesema kitendo cha wilaya ya Ngara kupangiwa kata sita pekee kinawanyima fursa ya walio wengi kutoa maoni yao ili katiba itakayoundwa iwahusishe watanzania wote.

Mmoja wa wananchi hao Bw James Bazitsa amesema ili wananchi kutoka kata nyingine waweze kutoa maoni katika kata jirani wanalazimika kutumia gharama kubwa jambo alilosema kuwa huenda likawawia vigumu baadhi ya wakazi wa wilaya hiyo.

Hata hivyo kaimu katibu tawala wilaya ya ngara Bw David Mafipa amesema kuwa kata sita zilizo katika ratiba ya sasa ni hatua ya awali na kwamba zoezi hilo litafanyika kwa miezi 18 .

Aidha Tume ya kukusanya maoni ya wananchi  juu ya kuundikwa kwa katiba mpya  imeanza  shughuli zake mkoani kagera kwa kuanzia wilaya ya  Biharamulo ambapo tume hiyo itakusanya maoni katika vituo viwili kwa siku na kwamba mikutano husika itafanyika kwa muda wa saaa tatu.

Wakazi wa wilaya ya Ngara wataanza kutoa maoni yao asiku ya alhamisi ijayo kwa kuanzia kata ya Muganza kabla ya wakazi wa Murusagamba kushiriki pia kutoa maoni yao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad