![]() |
Akizungumza na Waandishi wa Habari, makao makuu ya klabu makutano ya Mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam, Saintfiet alisema kwamba wachezaji hao watakuwa na timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, inayojiandaa mechi ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika Julai 29 dhidi ya Nigeria.
![]() |
Kocha Tom anasoma majina ya Kikosi cha Yanga |
“Kwa mujibu wa kanuni natakiwa kuwaachia wachezaji siku tano kabla ya mechi, na Jumamosi wanacheza na Rwanda, Jumatatu wanarudiana na Rwanda, baada ya hapo watakuwa kwenye maandalizi ya mechi na Nigeria, kwa hivyo sitakuwa nao hata kwenye Nusu Fainali, kwa sababu hiyo nimeamua kuwaacha,”alisema.
Kocha Saintfiet alisema amemtema pia Nahodha wa klabu hiyo, Nsajigwa Shadrack katika kikosi cha wachezaji 20, lakini amesema mchezaji huyo ni muhimu na atakuwa naye kwenye Ligi Kuu.
![]() |
Mchezaji Hamis Kiiza |
Amewataja wachezaji aliowateua baada ya kushauriana na wasaidizi wake, Freddy Felix Minziro na Mfaume Athumani kuwa ni; makipa Yaw Berko na Ally Mustafa ‘Barthez’, mabeki Juma Abdul, David Luhende, Kelvin Yondan, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Godfrey Taita, Ladislaus Mbogo, Oscar Joshua, Stefano Mwasyika, viungo Athumani Iddi ‘Chuji’, Rashid Gumbo, Juma Seif ‘Kijiko’, Haruna Niyonzima, Shamte Ally, Nizar Khalfan, Idrisa Assenga, Hamisi Kiiza na washambuliaji Said Bahanuzi na Jerry Tegete.
Yanga, ambao ndio mabingwa watetezi wa Kagame, watafungua dimba na mabingwa wa Burundi, Atletico FC Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
![]() |
| Makao makuu ya klabu ya Yanga , Jangwani Dar es salaam. |
KIKOSI
CHA YANGA KAGAME.









No comments:
Post a Comment