Baada ya Yanga kupigwa 2-0,Simba nae alizwa 2-0 na URA Taifa’katika KAGAME CUP - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, July 15, 2012

Baada ya Yanga kupigwa 2-0,Simba nae alizwa 2-0 na URA Taifa’katika KAGAME CUP


Mashabiki wa timu ya Simba wakiwa wamefurika katika uwanja wa Taifa kujionea timu yao ikicheza katika mechi zake mbalimbali.

Mashabiki wa Timu Vigogo hapa nchini  wamekuwa wakitoka Uwanja wa Taifa Mjini Dar es Salaam kwa masikitiko baada ya jana Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa michuano ya Kagame kuchapwa 2-0 na leo ikawa zamu ya mahasimu wao wakubwa Wekundu wa Msimbazi Simba kunyukwa Bao 2-0 na timu ya Mamlaka ya mapato kutoka Uganda URA katika Mechi ya kwanza ya Kundi A ya Mashindano ya kuwania Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Kagame CUP.


Bao za URA katika mchezo huo zilifungwa na Owen Kasule katika Dakika ya 11 na Feni Ally kwenye Dakika ya 92.


Katika Mechi nyingine ya Kundi A iliyochezwa mapema huko Uwanja wa Chamazi, kwenye Viunga vya Jiji la Dar es Salaam, matokeo yalikuwa Vita Club ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC  kuibuka na ushindi wa  Bao 7 na Ports ya Djibouti 0.


Wachezaji wa Azam FC

Baada ya Mechi hiyo, wakaingia wenyeji wa Uwanja wa Chamazi, Azam FC kucheza Mechi ya Kundi B  na Mafunzo ya Zanzibar  na matokeo yalikuwa Bao 1-1.

 

MECHI ZINAZOFUATA:

Julai 17 Jumanne

 

6 ATLETICO vs APR [Uwanja wa Taifa, Saa 8 Mchana]

7 WAU SALAAM vs YANGA [Uwanja wa Taifa, Saa 10 Jioni]

 

Jumatano Julai 18

 

8 VITA CLUB vs URA [Uwanja wa Taifa, Saa 8 Mchana]

9 PORTS vs SIMBA [Uwanja wa Taifa, Saa 10 Jioni]

 

Julai 19 Alhamisi

 

10 ATLETICO vs WAU SALAAM  [Uwanja wa Taifa, Saa 8 Mchana]

11 MAFUNZO vs TUSKER [Uwanja wa Taifa, Saa 10 Jioni]

 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad