Tukio hilo limetokea leo Jumapili majira ya saa 8:30 katika kijiji cha
Chibingo kata ya Katoro eneo ambalo mwaka jana kulitokea ajali ya basi la Bunda
na kuua watu 14 papo hapo na kujeruhi wengine 28.
Katika tukio hilo watu 9 wakiwemo watoto watatu wamekufa papo hapo,huku
wengine wawili mmoja akifariki njiani wakati wa kukimbizwa hospitalini huku
mwingine akifariki wakati akipatiwa matibabu na madaktari katika chumba cha
Upasuaji.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Geita Paul Kasabago amelithibitihishia
gazeti hili kuwepo kwa tukio hilo,na kueleza kuwa ajali hiyo ni mbaya nay a
kwanza kutokea katika kipindi cha mwaka huu huku akitaja magari yaliyopata
ajali kuwa ni zenye namba T 344 AZE zote aina ya Toyota Corola,na T 421 BHS
Toyota land Cruiser.
Aliwataja waliokufa papo hapo katika ajali hiyo kuwa ni Maria Elisante
(18) mkazi wa Mganza wilayani Chato,Masasila Benjamin (17) mkazi wa Mkolani
mjini Geita,James Ntungirwenge (36) Mkazi wa Nyankumbu Geita,na Eliud Ngovongo
(36) pamoja na watoto wake watatu Amin (10),Emison(7),na Sara(4) wote wakazi wa
Kalangalala mjini Geita.
Alisema bado majina ya marehemu watatu mpaka jioni ya jana yalikuwa bado
hayajatambuliwa,huku akibainisha kwamba tayari marehemu saba kati ya 11 waliofariki
wametambuliwa na ndugu zao.
Kamanda Kasabago alisema katika tukio hilo watu 12 wamejeruhiwa na
kulazwa katika hospitali ya wilaya ya Geita,huku wanne kati yao ambao hali zao
ilionekana kuwa mbaya wamekimbizwa katika hospitali ya rufaa ya Bugando kwa matibabu
zaidi.
Mganga mkuu wa Wilaya ya Geita Dk.Abdalah Dihenga jana aliwaongoza
madaktari wengine kutoa huduma kwa majeruhi,ambapo mwandishi wa Gazeti hili
aliwashuhudia wakitoa huduma kwa wagonjwa katika chumba cha upasuaji
hospitalini hapo.
Akisimulia tukio kamanda Kasabago alisema chanzo cha ajli hiyo mbaya ni
mwendo kasi wa magari mawili madogo ya abiria yajulikanayo kwa jina la
‘Michomoko’ ambayo yaligongana uso kwa uso na gari linguine aina ya Land
Cruiser.
Kamanda Kasabago alisema magari hayo mawili yalikuwa yakifukuzana kutoka
mjini Geita kwenda Katika mji mdogo wa katoro huku yakiwa na abiria,ambapo
baada ya kufika katika eneo hilomoja liliamua kulipita lingine na ghafla
likakutana na gari linguine mbele.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Magalula Said Magalula alifika katika chumba cha
kuhifadhia maiti katika hospitali ya wilaya ya Geita,na kushuhudia miili ya
marehemu iliyokuwa imelazwa chini katika chumba hicho.
Akizungumza na mamia ya wananchi waliokuwa wamefurika nje ya Viwanja vya
jingo hilo la kuhifadhia maiti katika hopspitali ya wilaya hiyo Mkuu huyo wa
Mkoa alitoa pole kwa wafiwa,na kuwataka kuwa na moyo wa subira wakati wa
maombolezo ya vifo vya ndugu jamaa na marafiki zao.
Source: mwanawaafrika.blogspot.com





No comments:
Post a Comment