Taswira Picha Magari 7 yakiteketea kwa Moto - Rusumo,Ngara mkoani Kagera. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, August 19, 2018

Taswira Picha Magari 7 yakiteketea kwa Moto - Rusumo,Ngara mkoani Kagera.

Moja ya Magari ya Kampuni ya Azam likiwa limeteketea kabisa kwa moto sambamba na trekta katika kituo cha forodha cha Rusumo Wilaya ya Ngara mkoani Kagera mpakani mwa Tanzania na Rwanda baada  ya gari la Mafuta ya petrol kupoteza mfumo wa breki na kuyagonga magari mengine yaliyokuwa yakisubiria utaratibu wa kuvuka mpakani kisha moto kulipuka na kusababisha mengine kupatwa moto huo.
Jumla ya magari 7 yameteketea kwa moto huo uliosababisha na Lori la Mafuta la kampuni ya Lake Oil na katika tukio lililotokeoa leo August 19,2018 majira ya saa 08:45 Asubuhi, na mtu mmoja ameripotiwa kufariki dunia na wengine kujeruhiwa.

Pichani ni Helkopta ya Kikosi cha zima moto toka Nchini Rwanda  kimesaidia kuuzima moto  huo, ambapo kwa mujibu wa mashuhuda waliokuwepo eneo la tukio wamesema kuwa moto ulikuwa mkubwa na kulikuwa na Hatari ya kuteketeza Ofisi za kituo cha forodha,Benki ya NMB na Magari mengineyo huku baadhi ya Wananchi wakijeruhiwa kutokana na kupata taharuki.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad