![]() |
Muonekano wa Magari Saba
ya mizigo na Trekta moja yakiwa yameteketea kwa moto katika kituo cha
forodha cha Rusumo
Wilaya ya Ngara mkoani Kagera mpakani mwa Tanzania na Rwanda baada ya
gari la Mafuta ya petrol kupoteza mfumo wa breki na kuyagonga magari
mengine yaliyokuwa yakisubiria utaratibu wa kuvuka mpakani kisha
moto kulipuka na kusababisha mengine kupatwa moto huo. Katika Tukio hilo lililotokeoa leo August 19,2018 majira ya saa 08:45 Asubuhi, Mtu mmoja ameripotiwa kufariki dunia aliyekuwa Dereva kwenye Lori lililosababisha ajali. |
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhWUlL1hsmOkI19YaliG4OdJyytuaw3AztcU3t8qLAMdrVo9iAQwEG1w-xhqXpoubKKwDy5fqYw-ijVzWq4Gl3d1RqmAtOhuc831Srs8IqKH4Tb1TTAUqPWAjVBJhRhNY9TS-TjCedrtBXW/s640/39453713_236664386924750_6762095655847460864_n.jpg)
![]() |
Helkopta ya Kikosi
cha zima moto toka Nchini Rwanda kimesaidia
kuuzima moto huo, ambapo kwa
mujibu wa mashuhuda waliokuwepo eneo la tukio wamesema kuwa moto ulikuwa
mkubwa na
kulikuwa na Hatari ya kuteketeza Ofisi za kituo cha forodha,Benki ya NMB
na Magari mengineyo huku baadhi ya Wananchi wakijeruhiwa kutokana na
kupata taharuki.
|
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhD59gy89RwuD8dgL-wnQAs2hObEZZqPevJmr6a5EXLvmz0Suu6O4XmHyDqhkn3dl0iqClS_cn5J6A30oQj12SKGPDWJlbRTRpHUqNcoMIzmZT7Nr9qvhiNlV5pTBWT5SeamIx-V_KuFknZ/s640/39515385_1982427555147781_5920340438731980800_n.jpg)
![]() |
Hata hivyo, Mkuu wa wilaya ya Ngara, Luteni Kanali Michael Mtenjele amesema ukosefu wa zimamoto ni changamoto kubwa wilayani Ngara kutokana na matukio ya ajali ya moto kuongezeka na ombi lilishatumwa serikalini lakini utekelezaji wake haujafikiwa. |
![]() |
Mkuu wa
wilaya ya Ngara Luteni kanali Michael Mntenjele ambaye ni Mwenyekiti wa kamati
ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo amesema utingo wa gari hilo alibahatika
kuruka na kuumia na amekimbizwa hospitali ya Nyamiaga kwa matibabu.
Wakala wa
forodha kituo cha Rusumo Abdul Shakuru amesema gari lililosabanisha ajali ni
mali ya kampuni ya Lake Oil na magari mengine ikiwemo kampuni ya Azam ambayo hufanya
shughuli zake za kisafirisha mizigo kutoka Tanzania kwenda nchini Rwanda.
|
No comments:
Post a Comment