![]() |
Mbunge wa Jimbo
la Ngara mkoani Kagera Mhe. Alex Gashaza leo August
17, 2018 ameshindwa kuzindua mradi wa maji wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Baramba
wilayani Ngara baada ya kuwempo Ukatikaji wa
nishati ya umeme mara kwa mara
katika wilaya hiyo.
|
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj3ChN_TEpRgHw-VqZW4s_k1gVmEeZkkBVvD3sxX9ivx3bsvAToo1pe7imrwqcS0d8VA3AqKmbDNcxTFY7jQMENXeWqQYpIPg4o27O7wyZqzAQnW8X_ephGTqDr3UE5F4GyrQwNhoM-zFPU/s640/39404647_1355234484606496_8630498028374982656_n.jpg)
![]() |
Mwenyekiti
wa Shirika la Marafiki wa Afrika Tanzania Padre
Isias Bambara amesema kukatika kwa umeme umekuwa ni changamoto ya
maendeleo kwa wanafunzi wa shule hiyo ambao
ni moja ya mradi wa shirika hilo wilayani Ngara
Amesema Shirika
la MAT lilianza mwanzoni mwa mwaka 1981 chini ya wamisionari wa kikatoliki kutoka nchini
Ujerumani likishirikiana na mapadre wa jimbo la Rulenge wakati huo wakiongozwa na marehemu Askofu Christopher Mwoleka kueneza injili ya
jumuia ndogondogo jimboni humo.
|
![]() |
Hata hivyo Mbunge
ameridhia kuendelea na shughuli nyingine
katika sherehe hizo ambazo zimehudhuriwa na watu mbalimbali kupata
taarifa za miradi ya kijamii hasa katika sekta ya elimu afya maji na
ujasiliamali katika mkoa wa Kagera.
Baada ya
zoezi hilo kukwama Mhe.Gashaza
aliendelea na shughuli nyingine kupata taarifa za utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya kijamii huku akikata utepe wa mnara wa kumbukumbu wa
marafiki wa afrika tangu kuanzishwa na kupata usajili mwaka 1997 katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Baramba wilayani Ngara.
Amesema
kukatika kwa umeme wilayani Ngara baada
ya kuingia katika mfumo wa gridi ya Taifa unasababishwa na kiwango kidogo
kinachotoka katika kituo cha gridi ya taifa wilayani Biharamulo hivyo kushindwa
kuhimili mahitaji ya wananchi
|
![]() |
Amesema eneo
ilipo shule ya wasichana Baramba makao makuu ya marafiki wa Afrika limenufaika na kituo kidogo cha Afya kwa
ajili ya wananjamii, na pamejengwa taasisi
kama kituo cha JWTZ ikiwemo shule
ya sekondari ya wavulana Lukole inayochukua wanafunzi wa kidato cha tano.
“Tunapoadhimisha miaka 20 ya MAT wananchi tujitahidi kutunza
miun dombinu iliyogharimu malilioni ya fedha zaidi ya Sh572 milioni kwa wilaya
ya Ngara na Sh102 milioni kwa wilaya ya karagwe na kunufaika nayo” Amesema Gashaza
Amewakaribisha
wafadhili kutoka Ujerumani kuwekeza miradi mbalimbali mkoani kagera kwa kutumia
vivutio mbalimbali kwa kufanya utalii wa ndani utamaduni wa kijadi utengenezaji
wa bidhaa za asili na kuongeza uzalishaji kiuchumi.
Shirika la
Marafiki wa Afrika Tanzania limetoa ufadhili
wa kuwasomesha watoto 85 yatima katika wilaya ya Ngara mkoani Kagera
kwa kugharimia mahitaji ya kielimu kwa thamani ya Sh116 milioni kati ya
mwaka 1997 hadi mwaka jana 2017 tangu kuanzisha miraji ya kijamii mkoani humo.
Katibu mtendaji
wa Shirika hilo David Bukozo ametoa
taarifa hiyo Agost 17 katika maadhimisho ya jubilee ya miaka 20 ya kuanzishwa
shirika la Marafiki wa Afrika Tanzania
(MAT) yaliyofanyika shule
yasekondari ya wasichana Baramba wilayani Ngara.
Bukozo
amesema sanjari na ufadhili kwa watoto
hao shirika hilo limetumia Sh102.6 milioni kufadhili miradi ya elimu,
kilimo,afya,ufugaji, elimu ya ufundi kwa vijana, wanawake wajane kabla na baada
ya kusajiliwa katika wilaya ya Karagwe
na kuanzisha miradi hiyo wilayani Ngara.
Amesema
miradi mingine iliyoanzishwa na kuendelezwa wilayani Ngara ya elimu Afya kilimo
ufundi na ujasiliamali kwa vikundi vyenye watu wa rika mbalimbali viligharimiwa
Sh455.8 milioni na kuwawezesha kujipatia
maendeleo.
"Mbali
na fedha za kugharimia miradi hiyo
marafiki wa Afrika kutoa Ujerumani walisambaza vifaa vya ufundi , dawa na vifaa tiba katika taasisi mbalimbali wilayani Ngara na kunufaisha wanajamii kupata
maendeleo”Amesema Bukozo.
Amesema
baada ya kuungana na kuanzisha ushirika
wa kichungaji mwaka 1997 walianzisha umoja huo kwa mikataba ya kulenga kutoa
huduma za kijamii katika sekta ya elimu, Afya, Maji, na kuwezesha watoto yatima
na wanaotoka mazingira magumu kupata njia za kuwakwamua na changamoto za
maisha.
|
No comments:
Post a Comment