Halmashauri ya Ngara Haina Uwezo kwa Sasa kununua Gari la Zimamoto - DC. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, August 21, 2018

Halmashauri ya Ngara Haina Uwezo kwa Sasa kununua Gari la Zimamoto - DC.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti ( mwenyeshati la pinki ) akitazama mabaki ya magari 6 na trekta moja yaliyoteketea kwa moto August 19,2018 katika kituo cha forodha cha Rusumo Wilaya ya Ngara mkoani Kagera mpakani mwa Tanzania na Rwanda baada  ya Lori la Mafuta kupoteza mfumo wa breki na kuyagonga magari mengine yaliyokuwa yakisubiria utaratibu wa kuvuka mpakani kisha moto kulipuka na kusababisha mengine kupatwa moto huo.
Kulia kwake aliyeshika fimbo ni Mkuu wa wilaya ya Ngara, Luteni Kanali Michael Mtenjele  sambamba na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bw.Aidan Bahama aliyesimama kushoto.
Gari juu pichani na Helkopta ya Jeshi la Zimamoto la Rwanda ikiwa angani eneo la Rusumo (Mpakani mwa Tanzania na Rwanda ) wilaya ya Ngara mkoani Kagera ikizima moto ulioteketeza magari sita na trekta moja na moto huo kusababisha kifo cha dereva na utingo kujeruhiwa hii jana August 19/2018.
Mkuu wa Wilaya Ngara Luteni Kanali Michael Mtenjele amesema kwa sasa Halmashauri ya wilaya hiyo haina uwezo wa kununua gari kwa ajili kuzuia majanga yanayotokana na moto kwani mapato ya ndani ya Halmashauri hiyo hayajitoshelezi.

Akizungumza na Redio Kwizera kwa mahojiano maalumu amesema bei kwa ajili ya kununua gari hilo ni kubwa na halmashauri haina uwezo wa kununua gari la Zimamoto.

Hata hivyo amesema tayari wilaya ya Ngara imeshapelekea ombi kwa Kamishna Mkuu wa Zimamoto kwa ajili ya kupatiwa gari hilo lakini hadi sasa hawajapata jibu lini wilaya itapatiwa gari hilo.

Kanali Mtenjele ametoa kauli hiyo kufuatia ajali ya moto iliyotokea August 19,2018 katika mpaka wa Rusumo ambapo malori sita na trekta moja yaliteketea kwa moto na kusababisha kifo cha mtu mmoja ambaye alikuwa ni dereva.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad