Watahiniwa wa shule ni 77,222 na wa Kujitegemea 10,421 kuanza Mitiani kesho Jumatatu Mei 7,2018. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, May 06, 2018

Watahiniwa wa shule ni 77,222 na wa Kujitegemea 10,421 kuanza Mitiani kesho Jumatatu Mei 7,2018.

Katibu Mtendaji wa Balaza la Mitihani la Tanzania (NECTA), Dkt. Charles E. Msonde.

Katibu Mtendaji wa Balaza la Mitihani la Tanzania (NECTA), Dkt. Charles E. Msonde leo May 6,2018 ameongea na wanahabari  jijini Dar es Salaam na kusema mitiani ya kidato cha sita (ACSEE) na Ualimu Utakaoanza kesho Jumatatu tarehe 7 hadi 25 Mei,2018.

Jumla ya Shule za Sekondari 674, Vituo vya Watahiniwa wa Kujitegemea 231 na Vyuo vya Ualimu 125 Tanzania Bara na Zanzibar ambapo Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limesema Watahiniwa 87,643 wanatarajiwa kufanya mtihani huo wa kidato cha sita.

Akizungumza na waandishi wa habari amesema kati yao watahiniwa hao, wa shule ni 77,222 na wa kujitegemea ni 10,421.

Dk Msonde amesema mtihani utafanyika sambamba na wa kozi ya Ualimu ambao Watahiniwa 7,422 wa Ngazi ya cheti na stashahada wamesajiliwa kuufanya.

"Maandalizi kwa ajili ya mitihani ya kidato cha sita na ualimu yamekamilika, ikiwamo kusambaza vijitabu vya kujibia na nyaraka zote muhimu zinazohusu mitihani hii," amesema Dk Msonde.






No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad