Bilioni 502 zatumika Miradi ya Kunusuru Kaya Maskini wilayani Ngara. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, May 22, 2018

Bilioni 502 zatumika Miradi ya Kunusuru Kaya Maskini wilayani Ngara.

Mkuu wa wilaya ya Ngara.

Jumla ya Miradi 1,704 yenye thamani ya shilingi bilioni 72 imetekelezwa na mpango wa kunusuru kaya maskini TASAF awamu ya kwanza na miradi 12,347 yenye thamani ya shilingi bilioni 430 imetekelezwa katika awamu ya pili.

Taarifa ya Mkuu wa wilaya ya Ngara mkoani Kagera Luteni Kanali Michael Mtenjele wakati akifungua mafunzo ya TASAF kwa wakuu wa idara mbalimbali katika ukumbi wa halimashauli wilayani humo.

Akina Mama wa Buhororo,Ngara wakisikiliza kwa makini maelezo juu ya Mradi.

Aidha Mratibu wa TASAF kutoka Makao Makuu Taifa Bw Yohana Issa Nchimbi amesema mafunzo hayo pia yatashirikisha madiwani na maafisa ugani ambao mara nyingi wanapata changamoto za walengwa walioko kaya maskini.

Mafunzo hayo yana lengo la kuwapa Wakuu wa Idara mbizu za utambuzi wa uwekaji akiba na kukuza uchumi wa kaya zinazonufaika na mpango wa kunusuru kaya maskini TASAF wilayani Ngara.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad