Kuokota Chupa kwa sasa ni Fursa ya Kipato. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, March 20, 2018

Kuokota Chupa kwa sasa ni Fursa ya Kipato.

Muonekano wa chupa za plastiki zilizokusanya  mtaani na kuhifadhiwa hapa eneo moja Rusumo,wilayani Ngara mkoani Kagera.
Hakika zamani ilikuwa ni laana kuambiwa utaokota Makopo. Siku hizi ni fursa ya Biashara inayokuza kipato cha wote wanaoweza kufanya hivyo.
Kutokana na maendeleo ya kiuchumi na ongezeko la uhaba wa ajira rasmi, hivi sasa kuna Wanawake, Vijana hata Wazee, wanaookota Chupa hizi kujipatia Kipato.
Kwa Mujibu wa Kiwanda cha Oak Hall cha Marekani kinachozitumia kuzalisha Nguo za aina mbalimbali, Chupa 27 zinatosha kutengeneza Joho Moja.

Kama ilivyo kwa Biashara nyingine, Changamoto hazikosekani. Wataalamu wa Afya wanasema umakini unahitajika kwa wote wanaojihusisha na Biashara hii hasa waokotaji.



Kwa mtazamo, Biashara ya chupa imesaidia kuimarisha usafi wa maeneo mengi nchini. 

Maeneo mengi sasa zaidi ya watu wanajishughulisha na uokotaji taka hivyo kupunguza kuzagaa kwake mtaani kwa kuziona ni fursa.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad