Klabu ya Simba SC inamsaka Mtoto huyu. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, November 12, 2017

Klabu ya Simba SC inamsaka Mtoto huyu.

Klabu ya soka ya Simba SC inamtafuta mtoto ambaye picha yake inasambaa mitandaoni akiwa amevaa  fulana iliyoandikwa jina la golikipa namba moja wa klabu hiyo Aishi Manula.

Taarifa ya klabu hiyo leo ambayo imetolewa kwenye ukurusa maalum wa klabu kwenye mtandao wa Instagram imeeleza kuwa mtoto huyo anatafutwa ili waweze kulipa fadhila kwa mpenzi yake aliyoyaonesha kwa klabu na golikipa.

Klabu ya Simba SC imekuwa na utaratibu wa kuwafikia watu wenye kwenda mbali zaidi katika kuonesha mapenzi na ushabiki wao kwa wachezaji na kikosi kizima cha Simba.

Msimu uliopita wa 2016/2017 Simba SC ilimtafuta kijana Aziz wa mkoani Dodoma baada ya kuonesha mapenzi yake kwa mshambuliaji Ibrahim Ajib ambaye alikuwa akichezea timu hiyo kabla ya kuhamia Yanga msimu huu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad