![]() |
|
ASKOFU Mkuu wa Kanisa la
Anglican Tanzania, Jacob Chimeledya -Pichani kulia, amewataka
Viongozi wa wanaotoa huduma za kiroho pamoja na Watendaji wa Serikali kutoa
huduma kwa Jamii kwa kutanguliza
moyo wa huruma na upendo katika kujenga misingi ya heshima na utawala bora.
Askofu Chimeledya ametoa wito huo
hii leo (Oktoba 29,2017) wakati wa ibada ya kumsimika Askofu wa nne wa Anglican
Dayosisi ya Kagera iliyoanzishwa mwaka 1985 kutoka dayosisi ya Viktoria Nyanza
-Mwanza
Amesema kila kiongozi wa kiroho
anafananishwa na Nabii Petro wakati akichunga kondoo wa mungu ambao ni waumini
chini ya usimamizi wa Yesu hivyo wachungaji na maaskofu wasitangulize tamaa,
uchonganishi na wawe wavumilivu katika kuongoza waumini wao
Akitoa mahubiri katika ibada hiyo
amemtaka askofu Bendankeha kufuata mafundisho na maelekizo ya kanisa anglikana
wakiwemo hata wapinzani wake ambao waliunda vikundi vya kupinga kusimikwa kwake
kuongoza dayosisi hiyo
Aidha amesema katika kuongoza kanisa
na dayosisi hiyo ahakikishe anatoa mchango wa kukemea vitendo vya unyanyasaji
wa watoto ambapo kwa sasa vitendo hivyo ni 38% hapa Tanzania
Alisema kila kanisa nchini watoto
wanne kati ya 100 wanakumbwa na kadhia ya unyanyasaji na ukatili kuanzia ngazi
ya familia na kwenye jamii hivyo kanisa kwa kushirikiana na vyombo vya dola ni
kuungana kupinga pia kutokomeza vitendo hivyo
"Watoto wanayo haki ya kuishi
kupata huduma za kijamii zikiwemo za kiroho kuwajengea misingi ya kupata malezi
na maadili mema yanaorandana na tamaduni za kitaifa" alisema
Chimeledya
Pia alisisitiza kujihadhali na
ubaguzi wa kikabila katika utoaji wa huduma bali uongozi wa aina yoyote
uzingatie misingi ya baba wa Taifa Hayati mwalimu Julius Nyerere ya umoja wa
kitaifa kwa makabila yote kutambuana kama taifa moja na kiimani yote yako chini
ya Mungu.
|
![]() |
|
Kwenye ibada hiyo,Waziri wa Katiba
na Sheria wa Tanzania Prof.Palamagamba
Kabudi amewataka Maaskofu wa Kanisa la Anglican nchini kutumikia waumini kama
mashemasi badala ya kuibua migogoro ya kugombania nafasi ya uaskofu na
kusababisha uvunjifu wa Amani, kiroho na kijamii.
Alisema katika kutumikia nafasi ya
kuwa askofu lazima kuzingatia miito ya mungu na Kristo kwani kikatiba
imeandikwa kila atimizaye miaka 65 anapaswa kumpisha viongozi mwingine hivyo
askofu mteule atumie kipaji taaluma na karama zake kuwsunganisha waumini na kanisa
ili kumtumikia mungu na waliomuweka katika daraja alilopewa
Alisema serikali inatambua mchango
wa madhehebu ya dini likiwemo kanisa la Anglican nchini katika utoaji wa huduma
za kiroho lakini na huduma nyinginezo za kijamii na kwamba serikali hiyo hiyo
inatafuta fursa za kupata fedha kuboresha miundombinu katika mazingira ya
wananchi mikoa yote nchini
Pia Waziri Kabudi alisema mojawapo
ya miradi mikubwa inayohitajo fedha kupitia mapato ya ndani kujenga reli
inayokwenda kupitia wilaya ya Ngara kuelekea nchi za Rwanda na Burundi huku pia
kujenga bwawa la umeme wamegawati 2100 ili kuwezesha hata kuchimba madini ya
nickel wilayani humo na kisha kuanzisha viwanda ili kuongeza ajira nchini.
|
![]() |
|
Naye askofu mteule Darlington
Bendankeha ameitaka serikali kuwalinda watanzania kwa kuimarisha ulinzi na
usalama kutokana na matukio ya uvunjifu wa amani ambayo kwa sasa
inaonekana kulegalega baada ya tukio kubwa la hivi karibu la kujaribu kuuawa
Tundu Lisu ambaye alijeruhiwa na kufifiza juhudi zake za kuwasemea wananchi
kukemea baadhi ya matendo ya ubadhilifu wa rasilimali za nchi.
Pia alisema Rais katika utendaji
wake na washauri alio nao kufikiria suala la kufufua mchakato wa katiba mpya
ambayo ni kiu kubwa ya watanzania kukuza demokrasia, haki za binadamu na
utawala bora ambayo katika kuleta maendeleo ya wananchi na uchumi wa taifa.
|
![]() |
|
Katika hatua nyingine,Askofu Chimeledya
alitumia nafasi yake kuipongeza serikali chini ya Rais Magufuli kudhibiti
ubadhilifu wa rasilimali za taifa ikiwemo rasilimali madini hivyo usimamizi na
mapato yasaidie kuboresha miundombinu ya kijamii kama maji afya barabara, elimu
na ujenzi wa reli nchini
Aliwataka watendaji wa serikali na
wanasiasa kufanya kazi kwa uadilifu badala ya kubeza juhudi za Rais anazofanya
na kufanya ubadhilifu kwa kuonesha uchungu na nchi yake katika kuongeza mapato
kiuchumi na hatimaye kuondoa umaskini na kujipatia maendeleo.
Alisema seikali iwe na matumizi bora
ya fedha zitokanazo na rasilimali kupitia vyanzo mbalimbali vya mapato na
kwamba kanisa la Anglican linaungana na juhudi zinazofanywa na Rais
Magufuli katika kuwakwamua wananchi kiuchumi akilenga kuondoa umaskini.
|










No comments:
Post a Comment