|
Watu watatu
wamekufa maji ndani ya Ziwa Victoria
katika Kisiwa cha Ilamba wilayani Muleba
Mkoani Kagera baada ya mtumbwi kuzama.
Watu hao
walikuwa wakitoka kuchota maji Kisiwa cha Mazinga. Mwili mmoja umeshaopolewa.
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Kagera, Augustino Olomi amesema watu hao walizama Jumatatu saa 6:30 mchana.
Amesema
miili ambayo haijapatikana ni ya Superius Severine (27) mkazi wa Kijiji
cha Nyakitaba na Evelius Zephrine (22)
wa Mubunda Kitoko wilayani Muleba
Kamanda
Olomi amesema mwili uliopatikana ni wa Adela Andrea (26), mkazi wa Kijiji cha Itongo.
Amesema
Nelson Boniphace (20), mkazi wa Kisiwa cha Ilamba aliogelea na kuokolewa.
Mtumbwi huo
uliokuwa na madumu 33 ya maji amesema unamilikiwa na Rashidi Sabini (33), mkazi
wa Kijiji cha Ilamba.
Amesema
mtumbwi huo kutokana na upepo ulipigwa na wimbi hivyo ulipinduka na kuzama.
|
No comments:
Post a Comment