
![]() |
|
Zaidi ya Ng'ombe 30 na kondoo saba wamekufa baada ya kupigwa na radi jana katika
jijiji cha Muhweza kata ya Mabawe wilaya ya Ngara mkoani Kagera ambapo radi hiyo iliambatana na mvua majira ya saa 11 jioni
kwenye kijiji hicho.
Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Muhweza
Bw.Alex Bahati Joseph amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba Ng’ombe hao walikuwa wanamilikiwa na
wakazi wa kijiji cha Muhweza na Mukalehe na walikuwa pamoja malishoni.
Bw Joseph amesema wamiliki wa mifugo
hiyo waliopata janga hilo wameachia
wanachi kujichukulia nyama bure bila kuwauzia na hakuna daktari wa mifugo
aliyefika jioni hiyo kutoa ushauri wa kitaalamu
juu ya uhalali wa kula nyama hiyo.
|

![]() |
|
Matukio ya radi kuua ng'ombe na mifugo mingine wakiwemo wachungaji wa
mifugo hiyo malishoni na hata binadamu wengineo hutokea kila mwaka katika
wilaya za Ngara , Biharamulo, Muleba na Karagwe mkoani Kagera pia hata katika wilaya inazounda mkoa wa Kigoma.
|









No comments:
Post a Comment