Spika wa
Bunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai amefunguka kuwa
wabunge wanaodai kuwa bunge ni dhaifu basi ni wazi watakuwa na mambo yanawasumbua
ndio maana wanatoa kauli za kudhihaki chombo hicho.
Mhe. Ndugai
amesema hayo jana mjini Dodoma baada ya kuwepo kwa baadhi ya wabunge wanaotoa
kauli zisizokuwa rasmi katika vikao vya bunge bila kufikiria kwamba
wanachokifanya hakina taswira nzuri kwa wapiga kura wao pamoja na kwa serikali
kwa ujumla.
"Yupo
mwenzetu alisimama hapa na kulalamika kuwa bunge hili ni dhaifu, kwa maoni
yangu hizi ni lugha za kuudhi kwa sababu wenzako wengi namna hii waliochaguliwa
na watu wakaletwa hapa halafu wewe unawaona kwa wingi wao ni dhaifu haipendezi.
"Unajua
sisi tunaokaa hapa mezani hatuchangii kama nyinyi, kazi yetu ni kuwapa
nafasi mseme, wakati mwingine zinatoka
shutuma ambazo hatuna nafasi ya kubishana au kulumbana lakini wakati mwingine
ni vizuri kutumia fursa hizi kusafisha baadhi ya mambo. Binadamu ni lazima uwe
na staha ile ndogo tu kuwaheshimu binadamu wenzako," alisema Ndungai
Pamoja na
hayo, Ndugai ameendelea kwa kusema "Katika bunge letu kinacholeta matatizo
humu ndani ni tabia na lugha, tukirekebisha hayo mawili tutaenda vizuri tu
lakini najua kundi hili ni kubwa hatuwezi kuwa wote tupo sawa, nitaendelea
kulisemea lakini pale kwenye ulazima tutachukua hatua.
"...Unapomwita
kiongozi ni dhaifu, maana yake unamlazimisha awe mkali, achukue hatua.
"Naona
wengine wanahaingaika sijui kufungua kesi....Lakini nasisitiza, Mimi ndio
Spika, nasema mwaka mtu hakanyagi hapa"
BOFYA PLAY
HAPA CHINI KUTAZAMA Mhe.NDUGAI AKIFUNGUKA ZAIDI.
|
No comments:
Post a Comment