Matokeo ya
kidato cha sita kwa mwaka 2017 yametoka leo Jumamosi, Julai 15,2017 huku shule
ya Wasichana ya Feza Girls ikiibuka
kinara kwa watahiniwa wake 67 kufaulu kwa kupata daraja la kwanza na la pili.
Shule
nyingine zilizoibuka kidedea katika matokeo hayo ni Marian Boys, iliyoshika nafasi ya pili, Kisimiri (Arusha) imeshika nafasi ya tatu na Ahmes (Pwani) imeshika nafasi ya nne.
Shule nyingine
ni Marian Girls (Pwani)
iliyoshika nafasi ya tano, Mzumbe
(Morogoro) nafasi ya sita, St Marry
Mazinde Juu (Tanga) nafasi ya saba, Tabora
Boys (Tabora) nafasi ya nane, Feza
BOYS (Dar es Salaam) nafasi ya tisa na Kibaha
ya Pwani iliyoshika namba kumi.
Shule kumi zilizofanya vibaya na
kushika mkia kitaifa.
Shule hizo
ni Kiembesamaki Unguja, Hagafilo (Njombe), Chasasa (Pemba), Mwenyeheri Anuarite
(Dar es Salaam) na Ben Bella (Unguja).
Nyingine
zilizotajwa kushika mkia ni Meta (Mbeya), Mlima Mbeya(Mbeya)
Nyingine ni Shule ya Sekondari ya Al-Ihsan
Girls (Unguja na St Vicent(Tabora).
|
No comments:
Post a Comment