Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akionesha Ripoti hiyo
ya Kamati ya pili ya Uchunguzi wa Madini yaliyo kwenye makontena yenye mchanga
unaosafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo ya madini sehemu mbalimbali
hapa nchini mara baada ya kukabidhiwa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Kushoto ni
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan na kulia ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
wakishuhudia.
|
Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi Tanzania, Mwigulu Nchemba.
Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba ametoa taarifa ya kumpongeza Rais wa
Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli kwa uamuzi aliochukua baada ya kupokea ripoti
ya pili ya mchanga wa madini.
Pamoja na
pongezi, Waziri Nchemba ametoa maagizo kuwa watu wote waliotajwa kwenye ripoti
hiyo wasiruhusiwe kutoka nje ya nchi isipokuwa kwa ruhusa maalum kutoka
serikalini na kuvitaka vyombo vya usalama kuhakikisha vinasimamia agizo hilo.
“Hakuna
uzalendo zaidi ya kulinda rasilimali za Taifa, Hakuna utetezi wa wanyonge zaidi
ya kulinda rasilimali zao.Hongera sana Mh.Rais kwa uzalendo wa vitendo kwa
Taifa letu.”
“Naelekeza
wote waliotajwa kuhusika hakuna kutoka nje ya mipaka ya nchi yetu isipokuwa kwa
kibali maalum kutoka serikalini. Vyombo vitekeleze maagizo ya Rais kwa utimamu,”
imesema sehemu ya taarifa ya Mwigulu Nchemba.
|
No comments:
Post a Comment