Ajali hiyo
ilitokea kilomita 100 baharini eneo la Kusini magharibi mwa mji wa bandarini wa
Yokosuka, nchini Japan saa nane unusu saa za Japan, jana Jumamosi.
Sehemu moja
ya meli hiyo iliharibika kabisa, lakini ikafaulu kurejea katika kambi yake
mjini Yokosuka, kwa msaada wa maboti ya jeshi la Marekani.
Kati ya
waliojeruhiwa ni kamanda wa meli ya Marekani ambaye alipelekwa hospitalini kwa
njia ya helikopta.
|
Uharibifu
kwenye meli ya mizigo ya ACX.
|
Waliojeruhiwa
wakiondolewa kutoka meli ya Japan.
Meli hiyo ya
kijeshi iligongwa na ile ya mizigo umbali wa kilomita 104 kusini magharibi mwa
Yokosuka.
Haijulikani
ni wapi meli hiyo ya urefu wa mita 154 ambayo ni ya kuharibu makombora ilikuwa
ikielekea wakati huo.
Meli ya
mizingo ya ACX Crystal yenye urefu wa mita 222 iliyokuwa ikipeperusha bendera
ya Ufilipo ilikuwa ikisafiri kati ya miji ya Japan ya Nagoya na Tokyo.
|
No comments:
Post a Comment