Waziri wa
Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi) George Simbachawene ametoa idadi ya wanafunzi
waliochaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha tano na vyuo vya ufundi kwa
mwaka 2017 huku jumla ya wanafunzi 2,999 wakiachwa.
Simbachawene
ametoa kauli hiyo leo mjini Dodoma wakati akizungumza na waandishi ws habari na
kusema kuwa ufaulu kwa mwaka huu umeongezeka kwa asilimia 3.75 ukilinganisha na
matokeo ya mwaka 2015.
Waziri
amedai kati ya wanafunzi 96,018 waliofaulu kwa daraja la kwanza hadi la tatu ni
wanafunzi 93,019 tu ndiyo waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo
vya ufundi.
Waziri
Simbachawene amesema kuwa jumla ya watahiniwa wote waliofanya mtihani wa kidato
cha nne kwa shule kwa mwaka 2016 ni 349,524 huku waliofanya mtihani wa
kujitegemea ni 47,751 ambapo watahiniwa waliofanya mtihani wa shule waliofaulu
kwa daraja la kwanza hadi la tatu ni 96,018 sawa na asilimia 27.60 ya
watahiniwa waliofanya mtihani Tanzania Bara.
Simbachawene
alisema kutokana na mwongozo wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wa Mei
15, 2017 jumla ya wanafunzi 93,019 ndiyo wenye Sifa za kuchaguliwa kujiunga na
kidato cha tano na vyuo vya ufundi kwa kuwa wamefaulu vigezo vyote vya msingi
kama vilivyoaibishwa na Wizara ya elimu sayansi na teknolojia ambapo kati ya
hao 92,998 ni wa shule na wanafunzi 21 ni wale waliosoma taasisi ya elimu ya
watu wazima.
Aidha
amewataka wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano kuwasili
kwa wakati katika shule walizopangiwa July 17 mwaka huu na kwamba hakutakuwa na
mabadiliko ya shule walizopangiwa.
"Na
kama kuna mwanafunzi ambaye hataripoti kwenye shule aliyopangiwa kwa muda wa
siku 14 nafasi yake itachukuliwa na mtu mwingine," alisema Simbachawene.
Kuangalia
majina ya wanafunzi na shule walizochaguliwa.
|
No comments:
Post a Comment