|
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na
Wanahabari Mkoani Dodoma kuhusiana na kufuta agizo lililotolewa jana March
16,2017 na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe kuhusu Wananchi wanaohitaji kufunga ndoa
kuanzia mwezi Mei mwaka huu,2017 kuwa na vyeti vya kuzaliwa.
Rais
Magufuli amefuta agizo hilo leo March 17, 2017 (Ijumaa) wakati akizungumza na
waandishi wa habari muda mfupi kabla ya kuondoka katika Ikulu ya Chamwino
Mkoani Dodoma na kurejea Jijini Dar es Salaam.
Amesema
Serikali haiwezi kuruhusu sharti hilo kutumika kwa kuwa litawanyima haki ya
kuoa na kuolewa Watanzania wengi ambao hawana vyeti vya kuzaliwa, huku
utaratibu wa kupata vyeti hivyo ukiwa bado unakabiliwa na changamoto nyingi kwa
wanaohitaji.
Amesema
mpaka sasa idadi ya Watanzania walio na vyeti vya kuzaliwa ni chini ya asilimia
20 huku wengi wao wakiwa ni wananchi waishio vijijini ambako ni vigumu kupata
vyeti hivyo, na wengine wakiwa ni waliozaliwa kabla ya kuanza kutolewa kwa
vyeti vya kuzaliwa nchini mwaka 1961.
|
No comments:
Post a Comment