|
Sakata la
Madawa ya kulevya limeendelea kugonga vichwa vya habari wiki hii ambapo
Jumatatu hii Jeshi la polisi limedai toka lianze operesheni hiyo tayari
limewakamata watuhumiwa 112 na kati ya hao 12 wamepandishwa mahakamani Jumatatu
hii kwajili ya kiapo cha kutorudia matumizi ya Madawa ya kulevya baada ya
kukiri kutumia.
Kati ya watu
hao 12 ni pamoja na Wema Sepetu, Romy Jones, Petit Man, TID pamoja na wengine.
Aidha Wema
Sepetu baada ya kiapo hicho atarudishwa polisi kwajili ya kuandaliwa shtaka
jipya linalomkabili la kukutwa na msokoto wa bangi nyumbani kwake.
Akiongea na
waandishi wa habari leo, Kamanda wa Polisi wa Kanda maalumu ya Dar es Salaam,
Simon Sirro amesema watuhumiwa wengi waliohojiwa walikiri kutumia Madawa ya
kulevya na kati ya hao walieleza watu ambao wanawauzia.
“Tumewakamata
watuhumiwa jumla 112 na tumekamata kete 299 zinazodhaniwa ni za Madawa ya
kulevya na kwa kawaida haya Madawa Mkemia Mkuu wa serikali yeye ndiye
atakayetuambia ni Madawa ya aina gani,” alisema Kamanda.
Aliongeza,
“Katika watuhumiwa 112, kuna watuhumiwa 12 tumewapeleka leo mahakamani,
tumewapeleka mahakamani kwa sababu sheria ya mwenendo wa mashtaka iko wazi
kifungu cha 73 na 74, huwa tunaweza kuomba kwa mweshimiwa hakimu kuwaombea
watuhumiwa kwa kiapo, kwamba hawa watuhumiwa tunataka wabadilishe tabia zao.
Tunawapeleka mahakamani ili wakae chini ya uangalizi wa jeshi la polisi na
mahakama kwa muda wa miaka 2 wasifanye makosa tena,”
“Kwa sababu
tulichokibaini kwa wote tuliowakamata wengine wanakiri na wamekwenda kuonyesha
hayo Madawa ya kulevya. Kwa hiyo kusudio la kwanza wawe chini ya uangalizi
wetu, na kusudio la pili la kiapo chetu waache hiyo tabia ili wabadilike wawe
raia wema, lakini la tatu tumeomba wale wanakuja kuripoti kituoni angalau mara
mbili kwa mwezi na lengo letu ni kuona hawa ndugu zetu ambao walikuwa wanavuta
madawa ya kulevya wamecha kabisa,”
|
No comments:
Post a Comment