|
Leo February
8, 2017 -Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul
Makonda ameingia kwenye awamu anayoiita ni ya pili kwa kutaja orodha ya
watu ambao watahitajika kufika Polisi Central Dar es salaam kusaidia taarifa na
maelezo kwenye mapambano ya kutokomeza dawa za kulevya Dar Es Salaam.
Kwenye
orodha hiyo iliyosambaa mitandaoni kwenye jina namba 54 kuliandikwa Philemoni
Mbowe na hivyo habari zikaanza kusambaa kwamba sio Freeman Mbowe aliyetajwa.
Jioni hii ya Leo,
Paul Makonda amewaambiwa Waandishi wa habari kwamba jina la kwanza kwenye namba
54 lilikosewa na inatakiwa kuandikwa Freeman Mbowe hivyo anaehitajika Ijumaa ni
Mheshimiwa Freeman Mbowe
|
No comments:
Post a Comment