![]() |
|
Walisema
lori hilo lilipofika katikati ya mlima liliacha njia na kurudi nyuma hatimaye
likaporomoka bondeni, huku mizigo ikiwaangukia watu hao.
Kamanda
Wakulyamba aliwataja waliokufa kuwa ni Jamal Hemed (40), mkazi wa Mlalo, Hassan
Rashid (33) wa Nyasa, Bisura Seif wa Kifungilo, Hadija Said wa Mhelo, Zuena
Juma wa Kwedege na Husna Athumani wa Hemtoye.
Alisema
majeruhi wa ajali hiyo walipelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Lushoto kwa
matibabu. Kamanda huyo alisema dereva wa lori hilo, Nassoro Athumani (25)
anatafutwa kwa kuwa alitoroka baada ya ajali.
Alisema
uchunguzi wa awali unaonyesha chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva na ubovu wa
gari.
|








No comments:
Post a Comment